Kwa niaba ya Tumaini Swahili Chapel - Chicago, ninakukaribisha katika Ibada ya Kiswahili itakayofanyika pale Lutheran School of Theology - Chicago, Juni 26, 2016 saa 9:00 alasiri.
Anuani ni 1100 East 55th Street,
Chicago, IL 60615.
Tutakutana katika orofa ya pili chumba nambari 201.
Tumebarikiwa na ugeni wa Askofu Dr. Owdenburg M. Mdegella wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Iringa. Yeye atakuwa mhubiri wetu.
Tafadhari usikose kufika, pia mwalike jamaa, rafiki na jirani mpate kubarikiwa. Mara tu bada ya ibada tutajumuika kwa viburudisho.
No comments:
Post a Comment