Wednesday, June 1, 2016

KASESELA AITISHA BARAZA LA BIASHARA LA WILAYA NA KUTOA MWELEKEO WA 2016/17

Mkuu wa Wilaya Mhe. Richard Kasesela.
Katibu wa sekretariat ya Baraza Bwana M. Sizya
Bwana B.M. Kunzugala akichangia hoja kueleza uanzishwaji wa mabaraza na umuhimu wake.

​Mkuu wa wilaya ya Iringa leo ameongoza Baraza la Biashara la Wilaya ya Iringa, katika hotuba yake ya ufunguzi alisisitiza mambo yafuatayo;

"Mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yanaamaanisha kuongezeka kwa kipato cha wananchi ambayo husababishwa na kukua kwa kipato cha wananchi. Kukua kwa ajira na kuongezeka kwa tija kwenye uzalishaji iwe kwenye kilimo au viwandani ndiko kunako leta mabadiliko ya kiuchumi. Ukuuaji huu huleta mabadiliko makubwa katika miji na kuibuka kwa miji midogo mipya. Haya yote kwa pamoja yanaleta changamoto katika utoaji wa huduma za jamii."

Mh Kasesela aliendelea kusema "Katika kuyatekleza mabadiliko ya kweli ili wilaya yetu ipande juu hatuna budi mambo yafuatayo tuyaboreshe kwa nguvu zetu zote, mambo hayo ni pamoja na ;

1. Uongozi bora pande zote mbili serikali na sekta binafsi. Sekta binafsi ni muhimu wakafanya chaguzi kuweka viongozi kutokana na weledi na serikali na sisi tutahakikishe tuna viongozi na watendaji wenye weledi na wenye maono ya mbali.

2. Kupanga na kutekeleza mikakati kwa umuhimu (prioritization), hatuwezi kukamilisha kila kitu kwa wakati mmoja lazima tujipange na tupange kwa umuhimu kwa kuzingatia rasilimali zilizopo.

3. Kuongeza tija katika uzalishaji Kukuza viwanda vilivyopo na kuongeza vipya, msingi mkubwa wa hili ni kuhakikisha viwanda vyetu vinatoa ajira na kujenga watu wenye kipato cha kati.

4. Mabadiliko ya dhati ya fikra, hili ndio la msingi zaidi, kwa kasi ya awamu ya 5 ni muhimu kila mmoja akahakisha anabadili fira yake hasa kuona kuwa kila analofanya zaidi ni kumkomboa mwananchi wa kipato cha chini, awe sekta binafsi au ya umma. Wote kwa pamoja tuhakikishe tunamkomboa Mtanzania maskini na si kujinufaisha wachache.

IDBC (wilaya ya Iringa) inahitaji kufanya nini 2016;

1. Kusimamia na kuhakikisha pato la mwana Iringa linaongezeka kufikia mwaka 2020 (kusimamia vikundi pamoja na kukuza biashara)

2. Kuongeza kasi kukuza manispaa ikiwemo kusisitiza uboreshaji wa mipango miji ili kuweza kuwa jiji kubwa Tanzania.

3. Kushinikiza uboreshaji wa miundo mbinu ikiwemo usafiri wa anga ili ifikie kiwango cha kimataifa. Ambapo mazao yataweza kusafirishwa nje.

4. Kukuza Utalii hasa kwa kuhakikisha barabara km 104 kwenda mbuga za wanyama inajengwa kwa kiwango cha lami.

5. Kuongeza kasi ya usafi katika wilaya ili mji uonekane na hadhi ya kimataifa na kupunguza magonjwa.

6. Kusimamia kilimo chenye tija kitakacho lisha viwanda.

7. Kusimamamia kasi ya uboreshaji elimu toka ya awali mpaka elimu ya juu hasa kuhakikisha shule zote za sekondari zimo kwenye mfumo wa ICT

8. Kusimamia uboreshaji wa huduma ya afya hasa kuhakikisha kila kijiji kina kituo cha afya, nia hasa ni kukaribisha sekta binafsi kwney maeneo yanye kipato

9. Kusimamia utunzaji wa mazingira hasa kupiga marufuku ukataji miti ovyo. Pia kulinda vyanzo vya maji.

10. Kuongeza idadi ya viwanda kwa kukaribisha wawekezaji. Ni muhimu mwaka huu tukashawishi wawekezaji kufungua viwanda 2 katika wilaya yetu.

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti Mwenza Bwana Mwakabungu ambaye pia ni mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Iringa, alisisitiza suala la nidhamu katika utekelezaji wa majukumu, aliwaomba watendaji wa serikali kubadilika na kufanya kazi kwa bidii.

Katika mkutano huo zilitolewa mada mbali mbali toka SIDO, TRA na asasi ya RUDI. yote haya yakiwa na nia ya kuboresha mazingira ya biashara mkoa wa Iringa

No comments: