Advertisements

Thursday, June 30, 2016

MAKONDA ASHUHUDIA MAZITO AMANAMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda 
By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wazazi waliolazwa wodi ya wazazi Hospitali ya Amana, wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaongezea jengo jingine ili kuwa karibu na watoto wao baada ya kujifungua.

Wazazi hao ni wale ambao wanajifungua na watoto kubainika kuwa na matatizo mbalimbali yakiwamo ya kitovu, hivyo kulazimika kukaa katika wodi hiyo kwa ajili ya mapumziko wakisubiri wapatiwe matibabu.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mbele ya Makonda aliyetembelea hospitali hiyo jana, Aisha Juma alisema hivi sasa wanalazimika kupanda ngazi kwenda jengo jingine kuwanyonyesha watoto wao ambao wako katika uangalizi maalumu.

No comments: