Friday, June 10, 2016

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE NA TAASISI YA GSM FOUNDATION WAKABIDHI MIFUKO 600 YA SARUJI SHULE YA MSINGI MBANDE

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (wanne kulia) na Meneja Mkuu wa GSM Foundation Shannon Kiwamba (katikati) pamoja na wadau wengine, wakikabidhi mifuko hiyo 600 ya Saruji kwa uongozi wa Shule ya Msingi Mbande leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema akiwa pamoja na uongozi wa Taasisi ya GSM Foundation wakiwa kwenye stoo ilipohifadhiwa saruji hiyo.


Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema kwa kushirikiana na Taasisi ya GSM Foundation wamekabidhi mifuko 600 ya saruji kwa Shule ya Msingi Mbande iliyopo kata ya Chamazi ikiwa ni jitihada za kuboresha elimu kwa kukabiliana na changamoto za Uwepo wa madarasa uliokuwa unaikabiri shule hiyo kwa muda mrefu.

Licha ya kukabidhi mifuko hiyo 600 ya Saruji Mkuu wa wilaya Mjema ameahidi kufanya jitihada za kutafuta madawati 400 kukabiliana na changamoto za wanafunzi. kukaa chini huku akiongeza kuwa atalishughulikia ipasavyo suala là Uhaba wa walimu kwa shule hiyo kwa kuongeza walimu 40.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Dauden Mwakyambiku amesema msaada huo unatija kwao kwani tangu kuanza kwa sera ya elimu bure kumekuwa na changamoto ya ongezeko la wanafunzi ambalo linahitaji madarasa, ambapo shule hiyo inawanafunzi 5,815 huku vyumba vya madarasa vikiwa 16 na serikali imeagiza kila chumba kukaa wanafunzi 45.
Sehemu ya wazazi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema.

No comments: