Bondia
bora kuliko wote duniani na mwanaharakati wa haki za binadamu
Muhammed Ali amezikiwa jana katika maziko ya binafsi yaliyohudhuriwa
na marafiki na familia.
Awali kabla ya maziko hayo maelfu ya mashabiki wa bondia huyo walipata fursa ya kukaa kando ya barabara katika mji aliozaliwa wa Louisville, huko Kentucky na kutoa heshima za mwisho wakati gari lililobeba mwili wake likipita mitani.
Tukio
hilo lilifuatiwa na hafla ya kumbukumbu ya Muhammed Ali ambapo watu
mashuhuri kadhaa walipata fursa ya kumuelezea Ali, kwa namna
mbalimbali walivyomfahamu katika maisha yake.
Aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton akisoma wasifu wa Muhammed Ali
Mike Tyson, Lenox Lewis na Will Smith wakwanza kulia walikuwa miongoni mwa waliobeba jeneza la Muhammed Ali
Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uingereza David Beckham ni miongoni waliohudhurisha maziko ya Muhammed Ali
No comments:
Post a Comment