Advertisements

Sunday, June 26, 2016

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MPANGO WA KITAIFA WA KITUO CHA MAWASILIANO CHA JESHI LA POLISI (CALL CENTRE)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.(PICHA NA IKULU)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akizindua Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uuzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Bias=fra jijini Dar es salaam.. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akimkabidhi tuzo ya ufadhili Bi. Edna Rajabu wa kwa niaba ya Shirika la Utangazaji la TBC wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest mangu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akimkabidhi tuzo ya ufadhili Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Bw. Elius Mwakalinga wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Kiongozi wa chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, akisalimia wananchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akisimama wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akihutubia uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendajiw a Superdoll, Seif Ali Seif.

JONAS KAMALEKI, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka jeshi la polisi nchini kuwadhibiti majambazi ipasavyo kwa kuwanyanganya silaha kwenye matukio ya kiuharifu ili kukomesha vitendo viovu katika Taifa.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usalama wa Jamii.
“Inashangaza jambazi anavamia kituo cha polisi anaua na anaondoka wakati polisi wapo na wana silaha na risasi wanazo lakini wanashindwa kumnyang’anya silaha,”alishangaa Rais Magufuli. 
Ameongeza kuwa ujambazi na vitendo vya uharifu nchini inabidi vikomeshwe mara moja ili watanzania waishi kwa amani na kufanya maendeleo kwani wananchi wanataka maendeleo.
Akiongelea kuhusu maslahi na vitendea kazi kwa jeshi la polisi, Rais Magufuli amesema kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo kuliwezesha jeshi hilo ili liweze kufanya kazi kwa ubora zaidi.
Rais Magufuli ameonyesha kuwa na imani na jeshi la polisi licha ya kuwa na kasoro ndogo ndogo kwa baadhi ya polisi ambao wanalichafua jeshi hilo.
Aidha ametoa agizo kwa TCRA kushirikiana na jeshi la polisi nchini ili kuweza kurekodi simu na kutoa print out mara moja tofauti na ilivyo sasa.
Kuhusu kundi la wafanyakazi wanaofanyakazi kwenye Dawati la Taarifa la polisi, Mhe. Rais amemtaka Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu kuwafikiria na kuwapatia posho ya kazi kwani kazi wanayoifanya ni ngumu mno na inahitaji umakini zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemwomba Mhe. Rais kuliongezea fedha jeshi hilo ili liweze kufanya kazi kwa ustadi zaidi na kukomesha vitendo vya uharifu nchini.
Makonda amelipongeza jeshi la polisi kwa kudhibiti matukio ya ujambazi hapa nchini hususan kwenye mabenki.
Mpango huu wa Usalama wa Jamii umezinduliwa leo na utadumu hadi 2019 na unatarajiwa kutoa matokeo makubwa ya kudhibiti uharifu nchini.

No comments: