Jumamosi (June 25th, 2016), Watanzania wa Minnesota walipata nafasi ya kujumuika katika sherehe ya kumuaga (Send Off Party) Grace January Carol na January M. na mpwa wa Lau katika ukumbi wa jumuiya ya mji wa Shoreview. Grace anatarajiwa kuolewa jumamosi ijayo (July 2nd, 2016) na Mtumishi Rafael Nobe Nyange anayeishi katika jimbo la jirani la Iowa, mjini Iowa City.
Sherehe ilihudhuriwa na Mr. Gaspar (Baba mkubwa) na Leonia Kebwe (Shangazi) kutoka Tanzania; pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wengi kutoka majimbo mengine ya hapa Marekani, baadhi yao wakiwa Pastor Dave & Caroline Mngodo, Tina na Wilfred Chacha, Mr &Mrs Chacha, Chisore Nyirenda, Anina Mbilinyi, Malaika Meja, Angela Machota, Kev Kyariga na Tina Msuya.
Familia ya Kyariga inapenda kutoa shukrani za pekee kwa Joy Catering LLC, EeKay’s Photography, Allan Kingdom, Tuma’s LLC (Decorations) Cake by Galaxy Creatons, DJ Erick Baruti, wanakamati wote wakiongozwa na Dr. Ndaga Mwakabuta, Mr. & Mrs. Kagaruki, Mr Charles Semakula na Pastor Andrea Mwalilino. Bila kusahau shukrani za dhati kwa watanzania wa Minnesota ambao walishiriki kikamilifu kwa hali na mali katika sherehe hii ya kumugaga Grace. Mungu awabariki!
Grace akimvua kiatu mume mtarajiwa na kumvesha kiatu kipya kama ishara ya heshima ya kumkaribisha mume mtarajiwa kwenye familia na kumtakia kheri na baraka njema popote waendapo.
Grace akipata ukodak na mpambe wake Jackline Shanalingigwa , hakika walikuwa ng'aring'ari kiroho safi, Kwa picha zaidi jitiririshe hapa chini uone watu walivyokuwa ng'aring'ari. Picha kwa hisani ya Emma Kasiga (Super Lady)
Mume mtarajiwa akisubiri kuingia ukumbuni na mpambe wake
Grace akimpatia hug mumewe mtarajiwa
Mume mtarajiwa akisubiri kuingia ukumbuni na mpambe wake
Grace akimsindikiza mume mtarajiwa kuchukua chakula. |
1 comment:
Hongera January!
Post a Comment