Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundtion, Salama akikabidhi baadhi ya Vitu vya msaada kwa Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga jijini Dar es Salaam leo wakati walipotembelea katika kituo hicho kilichopo karibu na kituo cha Polisi cha Hananasif jijini Dar es Salaam.
Wawakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama na Zaituni Ramadhani wakikabidhi mafuta ya kupikia kwa watoto kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga jijini Dar es Salaam leo.
Wawakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama na Zaituni Ramadhani wakikabidhi mafuta ya kupikia kwa watoto kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mwakilishi wa kampuni ya Shamo World Foundation amesema kuwa wameguswa kutoa msaada katika kituo hicho kwa kutenda matendo ya huruma wakati wa kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani kwa watoto kwa kuwa wanamahitiji mengi pia ni kuwapunguzia ugumu wa maisha walezi wa watoto hao.
Nae Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga amewashukuru kampuni ya Shamo World kuwaona kwa jicho la pekee na kwenda kuwapa msaada katika kituo hicho.
Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama amesema kampuni hiyo wamekabidhi Kg 50 za Mchele, Kg 50 za unga wa ngano na unga wa ugali, Kg 50 za sukari pamoja na Maboksi 15 ya Tende pamoja na mafuta ya kupikia.
Wawakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama na Zaituni Ramadhani wakiwa katika picha ya pamoja na walezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na watoto walio klatika kituo hicho jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment