Afisa Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali, International Organization for Migration,(IOM), Charles Mkunde akizungumza na vijana wa waliopo shuleni na wasiokuwa shuleni kuhusu faida za kiusalama za uhamiaji.
Shirika lisilo la kiserikali, International Organization for Migration,(IOM) limeendesha mafunzo ya siku moja kwa zaidi ya vijana 150 waliyopo katika Vyuo Vikuu,Sekondari na wale wa mitaani lengo ni kuwapa elimu na kufahamu faida za kiusalama za Uhamaji.
Akifungua mafunzo hayo katika, Hotel Coral Beach iliyopo Masaki jijini ,Afisa Miradi wa shirika hilo Charles Mkunde, amesema kuwa lengo la kuwakutanisha vijana hao ili kuwajengea uwezo wa kutambua mambo mbalimbali yatokana na Uhamaji na kujua faida na hasara zake.
“Uhamaji sio tatizo la nchi pekee, bali tatizo la ulimwengu mzima ni wajibu wetu kufanya hivi kila mara maana kundi kubwa la vijana wakielimishwa basi kama taifa tunaweza kupiga hatua moja mbele lengo kubwa ni kueleza maswala jinsi gani jamii inaweza kufaidika na uhamaji kwa fuata taratibu sahihi za kiusalama,unajua wengi utumia mwaya huu uhamaji kwa kufanya biashara haramu za utumwa katika mataifa mbalimbali iwapo kila kijana ataelewa kwa kina kuhusu mafunzo haya basi atapeleka ujumbe katika jamiii na kuwa barozi mzuri ili mwisho wa siku yatumike maamuzi ya kibusara kama taifa”alisema Mkunde.
No comments:
Post a Comment