Advertisements

Wednesday, June 22, 2016

SIKILIZA ALICHOSEMA MBATIA BAADA YA UKAWA KUFUNGA MIDOMO

2 comments:

Anonymous said...

Upuuzi mtupu kutoka kwa wapuuzi. Upinzani mlianza kugoma siku ya kwanza kabisa ya Magufuli kuingia bungeni na mkatoka au kutolewa ndani ya bunge huku mkizomea mbele ya wageni waalikwa wa nchi yetu kutoka mataifa mbali mbali na kuliaibisha Taifa. Sasa inashangaza sana kusikia ukawa wakiongozwaa na chadema kumlalamikia huyu dada wa watu na CCM kuwa ni chanzo cha kulipasua taifa wakati ni kwamba ukweli usiokuwa na kificho yakuwa ukawa na chadema wamekusudia kuivuruga nchi na Maghufuli na serikali yake wasipokuwa makini kushughulikia hawa wapuuzi kweli wanaweza kusababisha amani iliodumu siku nyingi nchini kutetereka. Demokrasia gani wanayoipigania wao bungeni wakati wao ni minority? Barack Obama analia usiku na mchana kutaka kurekibisha mswada wa uuzaji wa silaha kwa baadhi ya wananchi wenye matatizo lakini juhudi zake zinagonga mwamba na hii ni kwa sababu Chama chake hakina nguvu bungeni kutokana na kuzidiwa na republican kwa idadi ya wabunge. Sasa Tanzania raisi ni CCM na bungeni CCM wanamiliki bunge tena by far kwa idadi ya wabunge halafu ukawa wanataka wawe na haki sawa bungeni na CCM,jamani? Sasa kama hiyo ni demokrasia wanayoiota ukawa basi watanzania tuliowachagua hawa wabunge wa upizani basi hapana shaka tumeyachaguwa majipu kwani wakati huu ni wakati wa kumpa raisi wetu wa nchi kila aina ya sapota katika kuijenga nchi hasa kiuchumi na kimaadili ambapo kwa kweli hali ilikuwa mbaya. Hoja ya upizani yakwamba naibu spika ni mbabe ni hoja jipu kabisa tena la utosini. Ukweli ni kwamba naibu spika ni mwanadada msomi anajua exactly what she is doing na ndio maana kushindwa kwa hoja upizani bungeni ndiko kunakowafanya kuliona bunge kama kaa la moto. Wewe jiulize mwenyewe mtanzania wa ndani ya Tanzania na nje ya nchi ulishaona wapi wabunge ambao kiuhalisia ni wawakilishi wa wananchi ambao wametumwa na wananchi na wananchi walipigana kweli kweli kuwapeleka bungeni yaani wananchi wameshamaliza kazi yao kilichobaki wanasubiri matunda ya uteuzi wao kutoka kwa mbunge wao lakini cha kushangaza wabunge hao hao wanapigania kwa nguvu zao zote kulikimbia bunge na kwena kufanya maandamano na mikutano ya hadhara yaani kazi ya wabunge wa upizani siku zote ni kuwadanganya watanzania kuwa wanaonewa na CCM na huku wakilalamikia damu kumwagika lakini ukiangalia matamshi na kauli za upizani ni umwagaji wa damu mtupu na hapana shaka wao ndio chanzo kikuu cha damu zote za watanzania waliomwaga damu zao kwa kisingizio cha siasa. Wapinzani wa Ghadafi walilia sana yakwamba jamaa ni dikteta walisafiri na kuweka kambi nchi za nje zenye nguvu kuunda mikakati ya kumngoa mwisho ya siku jitihada zao zilizaa matunda na hapana shaka kama ni somo Libya ni chuo kikuu cha kuwasoma wanasiasa na tamaa zao za madaraka. Mifano ipo mingi jinsi gani wanasiasa duniani huwahadaa wananchi husika na dunia kupitia kilio cha demokrasi huku wao wenyewe na wanaowasapoti ni matapeli wakubwa wa demokrasia. Wao ukawa kama wameshindwa kukaa bungeni na kupambana kwa hoja za nguvu na CCM na kuamuwa kuingia mitaani na kupambana na CCM wajue kabisa huo ni upotofu uliopitiliza mipaka na damu yoyote itakayomwagika katika maandamano yao ya lazima wasije wakalia na CCM wakisema ndio walioimwaga damu. Kila kitu kina mipaka yake na CCM na serikali yake wanamipaka yao ya kujaribiwa, mipaka hiyo ikivukwa upizani msije mkailaumu serikali na Maghufuli wake.

Anonymous said...

Waacheni wasuse wenzao wanapitisha bajeti ujinga mtupu majimbo mnayotoka umeme haujafika eti unasusia bunge live huyo mwananchi wako asie hata na umeme atalionaje bunge? pigania maendeleo ya umeme kwanza ndio uzibe mdomo wa TV live?