Thursday, June 2, 2016

UPDATE: WABUNGE WOTE WA UPINZANI WATOKA NJE ASUBUHI HII WAKIPINGA NAIBU SPIKA KUENDESHA VIKAO VYA BUNGE

Wabunge wote wa vyama vya upinzani leo tena  wametoka nje kupinga Naibu Spika wa Bunge  Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.

Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge, wabunge hao wametoka nje  majira ya saa 3:00 asubuhi na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.

Kambi  upinzani  ilianza utaratibu huo juzi kwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya Dk. Ackson kuingia ukumbini.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, juzi alisema wataendelea kutoshiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika hadi pale "haki itakapopatikana."

2 comments:

Anonymous said...

Kwa kweli unaweza kusema watu wazima hovyo,nimeteleza ni wanaume wazima hovyo. Wakati mwengine itatulazimu kwenda kuingia katika siasa tena kwa mgongo wa upizani huko nyumbani ijpokuwa sio malengo, itakuwaje wanaume wazima wanatoka nje ya chombo cha juu kabisa cha kutunga sheria ya nchi yetu huku wakijikunyata kama vile kuku aliemwagiwa maji kwa kumuogopa mdada? Wewe kama mtanzania bila ya ushabiki wako wa kisiasa hawa watu wa upizani ndio wale wanaolialia kutaka kuingoza nchi yetu leo hii wanaufyata kwa mwanadada mmoja shupavu wanashindwa kukabiliana nae kwa hoja wanaamua kukimbia,vipi kama hawa wapinzani tungewakabidhi nchi yetu na hizi changamoto za kila aina ya majipu anazokabiliana nazo mwanamme wa shoka Magufuli,kweli hawa wapinzani wanamkimbia mwanadada,wanamuogopa hadi kuacha viti vyao, hawa wapinzani kweli wangekuwa na ubavu wa kuthubutu kutumbua kijipele japo cha udiwani? Wapinzani wanaonekana ni watu dhaifu waliokosa mwelekeo. Nasema waliokosa muelekeo sio waliopoteza kwa kuwa siamini kama akina Mbowe wanamuelekeo wa aina wowote kuanzia mwanzo ya wapi wanataka kuipeleka Tanzania? Wewe kwa mawazo yako kama John Pombe Magufuli angekuwa anaongoza upizani bale bungeni zidi ya serikali ya akina Mbowe angetoka bungeni kwa kumhofia mdada? Kubali au kataa huo ni uamuzi wako lakini nakuhakikishia Magufuli asingekusanya kundi lake na kutoka nje ya bunge? hata iwe vipi angepambana mpaka kieleweke isipokuwa ukitafakari kwa undani unakumbuka yakwamba aliesoma kasoma kwani mara nyingi tunasahau yakwamba Magufuli ni msomi tena wa kiwango cha juu kilichotukuka tofauti na wanasiasa wetu maigizo kiswahili kiengereza cha kuokoteza ili waonekane wasomi kumbe hamna kitu. kiengereza ni lugha kama kiswahili hata mtu asiekwenda shule kwa nchi kama uingereza au America ataongea tu sasa hizo mbwembe za wabunge wetu kuchanganya kiengereza kiswahili zinatoka wapi? Si bora wakiongea kusukuma,kihehe nakadhalika wananchi watawaelewa zaidi.

Anonymous said...

yaani imeanza kuuchukia upinzani acha yaani watu wazima hovyo jamani kama ni wazalendo basi na posho wasichukue maana hawatuwakilishi