Monday, June 6, 2016

Ushauri wa Zitto Kabwe kwa CCM na CUF kuhusu Zanzibar

1 comment:

Anonymous said...

Sababu kubwa ya Zanzibar kushindwa kumaliza mkwamo wa kisiasa visiwani humo ilikuwa ni CUF kutokuwa tayari kwa suluhisho lolote lile lisilohusisha kutambuliwa kwa uchaguzi wa October 25, 2015 uliofutwa. Kama wakati ule wangekubali kurudiwa kwa uchaguzi huku wakiweka masharti fulani fulani ingekuwa rahisi zaidi kumaliza ule mkwamo kuliko sasa hivi kufikia muafaka wa serikali iliyowekwa madarakani kufuatia uchaguzi wa marudio wa March 20, 2016 kukaa pembeni kuwezesha uchaguzi mwingine kufanyika!

Hili jambo si rahisi kama wapiga porojo wa majukwaani wanavyoona, kwa sababu ni lazima kwanza Katiba ya Zanzibar ifanyiwe madiliko ya kuwezesha hilo kufanyika. Mwenye kuweza kufanya madiliko hayo ni BLW, ambalo wajumbe wake wote sasa hivi ni wanachama wa CCM. Ni wanasiasa wangapi (wa CCM au upinzani) visiwani humo wenye ujasiri kama huo wa kuweka maslahi yao pembeni kwa maslahi mapana ya Zanzibar? Ni lazima tukubali ukweli mgumu kwamba hiki kitu hakiwezekani! Sipendi kusema hivyo, lakini ukweli ni kwamba CUF wasipotafuta njia mbadala, ambayo ni more realistic, hii itakuwa imekula kwao mpaka 2020!