ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 1, 2016

AJALI INAYOHUSISHA MAGARI MATATU YAUA WATU 11 MKOANI MOROGORO

Habari iliyoripotiwa kupitia kituo cha ITV ni kuhusu ajali ambayo imetokea eneo la Veta Dakawa mkoani Morogoro ikihusisha magari matatu ambayo ni lori la mafuta, Lori lililokuwa limebeba kontena lililobeba mchele pamoja na basi la abiria mali ya kampuni ya OTA lililokuwa likitokea Bukoba kwenda Dar es Salaam.

Taarifa hiyo inasema kuwa watu 11 wamefariki dunia na wengine ambao idadi yao bado haijajulikana wamejeruhiwa.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro ameagiza jeshi la polisi kuweka usalama hasa kwenye eneo la tukio ili kuzuia wizi kwa majeruhi wa ajali hiyo. Pia Jeshi la polisi limekataza watu kuchota mafuta yaliyomwagika katika eneo la tukio ili kupunguza madhara zaidi.

Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi

No comments: