Advertisements

Saturday, July 23, 2016

DC AWAWEKA NDANI MAAFISA AFYA KWA KOSA LA KUKAIDI AMRI YAKE

Mkuu wa wilaya ya kahama DC Fadhili Nkulu Akiongea na waandishi juu ya uhamuzi wake wa kuweka rumande Mtendaji wa kata na Afisa Afya wa Mji

KAHAMA 
NA MOHAB MATUKIO

MKUU wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu amewaweka mbaroni Maafisa afya wa Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa kosa la kuacha uchafu ulikokuwa katika Barabara kuu ya Mji wa Kahama ya kwenda katika Nchini za jirani za Rwanda na Burundi hali ambayo imesababisha eneo hilo kuwa mrundikano mkubwa wa taka zilizokuwa zikitoa harufu mbaya.

Maafisa Afya hao waliowekwandani na Mkuu huyo wa Wilaya ni Johanes Mwebesya na mtendaji wa kata ya nyasumbi Enocent kapeli kwa kosa la kutoa uchafu hulioko mwanzo wa barabara kuu ya kuingia katika mji wa kahama eneo la Phatom na kuacha wanachi wakitupa taka katika eneo hilo ambalo halistahili.

Tukio hilo limetokea jana wakati Mkuu wa Wilaya ya Kahama
Fadhili Nkulu akipita eneo la phatom akielekea halmashauri ya ushetu kwa ajili ya ziara ya kikazi za kawaida na kuona lundo la uchafu katika barabara hiyo kuu ya kuingia Kahama Mjini jambo ambalo linalita sura mbaya kwa mji wa Kahama.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya Fadhili Nkulu alisema alitoa maagizo kabla ya kuondoka kwenda Halmashauri ya Ushetu mbele ya Mkurungezi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba pamoja na Mtendaji wa kata hiyo na afisa afya wa kata hiyo kuwa akirudi kutoka Ushetu akute uchafu huo umeondolewa hapo haraka sana jambo ambalo halikutekelezeka.

Nina waambia nyinyi maafisa Afya nikirudi toka ushetu jioni nikute lundo hilo la chafu limeondoka eneo hilo na pawe safi sitaki kuona takataka katika eneo hilo kwani hapo ni katika sura ya Wilaya ya Wilaya hata mgeni akija katika Mji wa Kahama cha kwanza kuona ni uchafu uliopo eneo hilo”, Alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu.

“Watumishi hawa wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Wamezoea kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wananchi haiwezekani mwanzo tuu wa kuingia Mjini wa Kahama kunakutana na Dapo la uchafu je huko ndani kutakuwa na hali gani kama mwanzo tu kunakuwa na Mrundikano wa taka kiasi hicho.”Alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.

Hata hivyo alisema kuwa wito wake kwa sasa kwa watumishi wa umma ni kuacha mara moja kufanya kazi kwa mazoea na kuakikisha kila moja wetu anatunza maeneo yake ya kazi na kufanya usafi katika maeneo yaliomadhubuti kwa hali ambayo itachangia kiasi kikubwa kuuweka Mji wa Kahama katika hali ya usafi hali ambayo inaweza kuchangia katika kuzuia magonjwa ya milipuko kama pikindupindu .


Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu pia aliwataka Watumishi wa Serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani Serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli na kauli yake ya hapa kazi inatakiwa kila mtumishi ajitume katika kufanya kazi za kuwahudumia Wananchi hali ambayo italeta mabadiliko makubwa katika utendaji wa kazi.

Mwisho

No comments: