Advertisements

Friday, July 15, 2016

JARIBIO LA MAPINDUZI WATU 42 WAPOTEZA MAISHA UTURUKI

 Jumla ya watu 42 wamepoteza maisha baada ya kundi moja la kijeshi nchini Uturuki kufanya jaribio la mapinduzi usiku wa kuamkia leo. Pia taarifa kutoka nchini humo zimesema kwamba wanajeshi hao wamekatwa 120, wakijaribu kufanya mapinduzi hayo kwenye Ikulu ya Uturuki.
 Vyombo vya habari Uturuki vimetangaza kwamba maofisa wengi wakuu wa jeshi, akiwemo mkuu wa Jeshi Jenerali Hulusi Akar wametekwa wakiwa katika makao makuu ya jeshi Ankara.
Kutokana na tukio hilo madaraja jijini Istanbul yamefungwa na ndege za kijeshi zikionekana kupaa katika anga ya Ankara.
 Kwa mujibu wa kituo cha CNN Waziri Mkuu Binalo Yildirim ametangaza kuwepo kwa hatua zisizo halali zilizochukuliwa na jeshi hilo na kusisitiza kuwa hakuna mapinduzi ya kijeshi.Amedai kwamba serikali bado inadhibiti nchi.
Hata hivyo magari yamezuiwa kuvuka katika madaraja yanayovuka mto Bosphorus jijini Istanbul huku bado risasi zikirindima katika mji mkuu huo.
 Kituo cha CNN Idhaa ya Uturuki kimeripoti kuwa Rais Recep Tayyip Erdogan yuko salama.
Mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na YouTube ilizimwa muda mfupi baada ya taarifa za mapinduzi ya serikali kutokea
 Rais wa Marekani Barack Obama ameungana na viongozi wengine kuhimiza utulivu nchini Uturuki baada ya kundi la wanajeshi kutekeleza jaribio la kupindua serikali.
 Obama amehimiza pande zote Uturuki kuunga mkono "serikali iliyochaguliwa kidemokrasia Uturuki, kuonyesha uvumilivu, na kujizuia na vurugu au umwagikaji wa damu’’Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani imesema
 Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry, naye amesema anatumai kutakuwa na uthabiti, Amani na uendelevu.
Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov amesema Urusi inawasiwasi na ingetaka kuona Uturuki ikirejea katika njia ya uthabiti na utawala wa kisheria
Runinga ya Taifa ya Uturuki, iliyotumiwa kutangaza mapinduzi, ilifungwa kwa muda ingawa baadaye ilirejea hewani pia Mitandao ya kijamii pia ilifungwa, ingawa haikubainika ni nani aliyeifunga.
 Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim, akiongea kwenye runinga, amesema kulikuwa na kundi jeshini lililotaka kupindua serikali.


No comments: