ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 30, 2016

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI LAFANYA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU SALAMA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto mstari wa mbele) akiwaongoza Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo kuelekea katika viwanja vya kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala eneo lililotengwa kwa ajili ya zoezi la uchangiaji damu salama mara baada ya kuwasili kituoni hapo mapema leo asubuhi.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye awaongoza viongozi waandamizi, maafisa, askari na watumishi wote wa Jeshi hilo katika zoezi la uchangiaji damu salama ili kutimiza dhima ya kuokoa maisha ya watu wanaopoteza maisha kwa ajali za moto, ajali za barabarani, vifo vya mama wajawazito wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua na magonjwa mbalimbali kama vile ukimwi, malaria, anaemia na kansa.

zoezi hili limefanyika katika viwanja vya kituo cha jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa ilala kwa kushirikiana na taasisi ya mpango wa damu salama ulio chini ya wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia watoto na wazee.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akihutubia Maafisa, Askari na watumishi wote wa Jeshi hilo wakati akifungua zoezi la uchangiaji damu salama ambalo lilishirikisha vituo vyote vya Zimamoto mikoani, ufunguzi huo ulifanyika katika viwanjwa vya Zimamoto na uokoaji mkoa wa Ilala mapema leo asubuhi.
Maafisa, Askari na watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka katika vituo vya Zimamoto Makao Makuu, Chuo, Ilala, Kinondoni, Temeke na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakimsikiliza Kamishna Jenerali (hayupo pichani )wakati akihutubia katika ufunguzi wa zoezi la uchangiaji Damu salama lililofanyika katika viwanja vya Zimamoto mkoa wa Ilala.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akichangia damu katika zoezi lililofanyika viwanja vya kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala zoezi lililoshirikisha vituo vyote vya Zimamoto mkoa wa Dar es Salaam mapema leo.
Askari na watumishi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakichangia damu katika zoezi hilo mapema leo asubuhi. (PICHA ZOTE NA FC GODFREY PETER)

No comments: