Advertisements

Thursday, July 7, 2016

Kichupa cha leo Rama Dee ft Young Yuda----- Mazoea
Mzuka wa Mazoea inaonyesha kiasi gani @Rama dee ni mtu wa kuthubutu sana. Rama Dee kafungua ukurasa mpya kwenye kitabu cha tasnia ya mziki wa kizazi kipya.
Kuingiza uimbaji wake na kwenye maudhui ya mziki uliotengwa sana Bongo na aina pekee ya muziki ilopata kufungiwa Tanzania, Mnanda(mchiriku) ni kuonyesha ujasiri wa hali ya juu kwenye sanaa.

Tuunge mkono harakati zake, kama we' ni shabiki na mpenzi wa muziki, tafadhali tazama Mazoea, ipe dole gumba na kuacha nasaha zako kule youtube.
Isambaze kwa watu wako wote mtandao.

Jamii ya sanaa na muziki tuna nguvu kuliko tunavyofanywa tuamini na hizi mamlaka zilizopo. Tuchukue mamlaka yetu wenyewe kivyetu. Twend'zetu wapwa.

No comments: