ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 3, 2016

MAGUFULI: ATC KUPAA TENA SEPTEMBA

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa shirika la ndege la Tanzania litarejea angani ''kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016''.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu ya Tanzania bw Gerson Msigwa

''Dkt. Magufuli amesema serikali yake imechukua hatua madhubuti za kulifufua shirika la ndege la Taifa.

Tayari mipango imefanywa kuhakikisha ndege mbili aina Bombadier Q400 zinanunuliwa na zitatua hapa nchini kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016.'' taarifa hiyo inaeleza.

Tamko hilo ni ishara nzuri kwa sekta ya uchukuzi nchini Tanzania na vilevile kanda nzima ya Afrika Mashariki ambayo imekuwa ikikabiliwa na gharama za juu za usafiri kutoka kwa mashirika ya kigeni.

BIASHARA NA RWANDA

Wakati huohuo rais Magufuli aliueleza ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Rwanda kuwa China imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania kujenga reli ya kisasa yaani “Standard Gauge” kwa nia ya kurahisisha uchukuzi wa mizigo kutoka bandari ya Dar es salaam kwa manufaa ya wafanyabiashara.Image captionMarais Paul Kagame na mwenyeji wake John Magufuli

''Tanzania imeamua kuipatia Rwanda eneo la kujenga bandari kavu kwa ajili ya mizigo ya wafanyabiashara wake na pia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) itafungua ofisi mjini Kigali nchini Rwanda ikiwa ni juhudi za kurahisisha na kuongeza biashara kati ya nchi hizi mbili.''

Juhudi hizo bw Magufuli anasema ni kuwahakikishia wafanyabiashara wa Rwanda kuwa bandari ya Dar es salaam ni salama kwao kupitisha mizigo na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha bandari hiyo na kurahisisha biashara kati ya nchi hizi mbili.

Kwa upande wake rais Paul Kagame wa Rwanda alitoa wito kwa ''Tanzania na Rwanda pamoja na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana na sekta binafsi katika kutumia fursa nyingi za kibiashara zilizopo baina yake na kuwaletea manufaa wananchi''.

BBC

3 comments:

Anonymous said...

Mtu wa vitendo kwakweli. Magufuli ni hazina kubwa ya Tanzania iliobarikiwa ukiachilia mbali gas na utajiri mwingine unaodhidi kuvumbuliwa Tanzania katika miaka ya hivi karibuni lakini Magufuli ni rasimali namba moja na hazina kubwa ya Tanzania na jitihada kubwa zinatakiwa kufanywa na kila mtanzania mwenye kuitakia mema Tanzania kuhakikisha anatunzwa na kulindwa ili afanye kazi yake na kuwatimizia watanzania yale yote wanayotarajia kutoka kwake.Tusipompa nafasi yake ya kufanya kazi kikamilifu inamaana yakwamba watanzania ni wanafiki yakusema tunataka kujikomboa na umasikini kwani jamaa ni kiboko ya viboko katika utendaji kama Eduwadi Lowasa alivyokwisha kusema Magufuli ni mwanamme hasa ni dume la n'gombe si mchezo. Huyu mtu ana nusu mwaka tu lakini kasi yake hata viongozi wa nchi zilizokwisha endelea wanapagawa na jinsi anyoitengeneza Tanzania. Nakumbuka wanaita Maghufuli style(what would you do if you are Maghufuli)? Of course country and its people come first than your personal interest if you are a civil servant. Hivi karibuni wazir mkuu wa uengereza alitekeleza kwa vitendo Maghufuli style alipoamua kumnunulia mkewe gari la kawaida sana tena second hand nakuacha magari ya thamani yanayolingana na hadhi ya mke wa waziri mkuu tena wa uengereza kiasi cha kumshagangaza, a car dealer kiasi cha kutoamini alichokuwa anashuhudia.kumbuka waziri huyo mkuu wa uengereza aliwahi kuulizwa kama angelikuwa yupo tayari kupita mitaani kuokota taka na kufanya usafi kama Maghufuli? Wapinzani Tanzania wapo na wivu na jinsi Magufuli anavyochapa kazi lakini njia wanazojaribu kuzitumia kumpunguza kasi kwa maslahi yao binafsi hasa ya kisiasa ni za chuki zaidi na hazina nia njema kwa watanzania waliowengi. Kumpiga vita Magufuli sawa sawa na kwenda kunwaga zege kwenye chanzo cha maji kinachotegemewa na wananchi katika ardhi inayonyeshewa na mvua baada ya ukame wa muda mrefu sasa tujiulize kama hao wamwaga zege wanania njema licha ya kuwa labda na sababu zao za msingi yakwamba wanataka kuzuia mafuriko yasije mitaani na kuleta athari, lakini na tija zaidi wanatakiwa waiwachie hiyo mvua inyeshe kwanza na kuangalia uwezo wake. Ni sawa kabisa na jitihada za upizani kutaka kumzima Magufuli na serikali yake hata mwaka hajatimiza, tunaimani yakwamba watanzania waliowengi watasimama kidete kumsapoti muheshimiwa raisi na azma yake njema ya kuwaletea maendeleo yao.

Anonymous said...

Sasa Watanzania Kilichobaki au kitu kinachotakiwa ni tuugane kwa pamoja na kuwakemea vikali wanaojaribu kumpinga Rais wetu maana hao watu hawaitakii mema nchi yetu ! Kwa maana nyingine hao ndio Adui wakubwa wa Taifa letu . Yaani ni Majipu, Maradhi,yanatakiwa kutumbuliwa na kutokomezwa kabisa! " TUNA IMANIII NA. MAGUFUUUULIIIIIIII!! OYAAAA OYAAA!! MAGUFULIIII!!! KWELIIII!!! KWELIII !!!

Anonymous said...

Punguza mahaba Ndugu...