Advertisements

Saturday, July 23, 2016

MAJERUHI USAIN BOLT ASHINDA MBIO ZA MITA 200

Usain Bolt ameonyesha kuboreka afya yake kabla ya michuano ya Olimpiki mwezi ujao, baada ya kushinda mbio za mita 200 katika uwanja wa Olimpiki wa London.

Bingwa huyo wa Olimpiki mara sita alitumia muda wa sekunde 19.89, akiwa mbele ya mwanariadha wa Panama Alonso Edward aliyeshika nafasi ya pili.
Muingereza bingwa wa medali ya fedha ya Jumuiya ya Madola Adam Gemili alishika nafasi ya tatu akitumia muda wa sekunde 20.07.

Uwezo wa Bolt kufanya vyema ulikuwa ukitiliwa shaka baada ya kutoweza kushiriki majaribio ya kufuzu kushiriki michuano ya Olimpiki, kutokana na jeraha.

No comments: