Advertisements

Thursday, July 7, 2016

MHE. BALOZI TUVAKO MANONGI ASHIRIKI SHEREHE ZA EID EL FITR NEW YORK


Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Mhe Tuvako Manongi akiongea kwenye hafla ya Eid Mubaraak iliyo andaliwa na waislam wa New York siku ya Jumatano. Mhe Balozi alipata mwaliko wa kufutari pamoja na waislamu kwenye sikuku ya Eid iliyofanyika kwenye viunga vya 30 Over Hill. RD. Mt. Vernon. NY.

Mwenyekiti wa kamatia ya Eid Bwana Seif akida akiongea kwenye hafla hiyo ya Eid ambayo ilifana saana watoto walipata zawadi mbali mbali na chakula kilikuwa cha kutosha.
Mhe. Balozi akiongoza Watanzani kuchukua chakula kwenye hafla hiyo ya Eid Mubaraak

Mwanamkasi mama mapishi mwenyewe akipata ukodak na Miss Mahundi
Hii ndiyo ilikuwa ng'aring'ari ya siku, kwa picha zaidi jitiririshe kwenye soma zaidi


Ustadh Amir kutoka New Jersey akiwa kwenye vazi nazifu kabisa No comments: