Advertisements

Saturday, July 30, 2016

Mwanafunzi Mtanzania Ashinda Insha ya Umoja wa Mataifa

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Mogens Lykketoft akiwazungumza washindi 60 wa Insha kuhusu Lugha Nyingi, Dunia Moja, miongoni mwa washindi hao ni mwanafunzi wa Kitanzania Amani Alfred Naburi anayesoma Chuo Kikuu cha African Leadership kilichopo nchini Mauritius wengine katika picha ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma ya Umoja wa Mataifa, Bi. Cristina Gallach.
Amani Alfred Naburi akisoma sehemu ya Insha yake aliyoiandika kwa lugha ya kiingereza ambayo ilizungumzia lengo namba kumi na moja la maendeleo endelevu ambalo linahusu Miji jumuishi, salama na endelevu. Hafla hii ilifanyika siku ya Ijumaa katika Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
Naburi anaonekana katika mstari wa tatu akishangilia jambo na wanafunzi wenzie kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao walikusanyika siku ya Ijumaa baada ya kushinda uandishi wa Insha kwa kutumia lugha sita rasmi zinazotumika katika Mikutano ya Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya wanafunzi wa Insha kuhusu Lugha Nyingi, Dunia Moja wakiwa katika ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa..Hafla hii ilikuwa ni sehemu ya Kongamano la Kimataifa la Vijana.

Na Mwandishi Maalum, New York

Mwanafunzi wa Kitanzania, Amani Alfred Naburi, ni mmoja wa kati ya wanafunzi 60 kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali duniani ambao wameshinda shindano la Insha ijulikanayo kama “Lugha nyingi, Dunia Moja” ( Many languages, One World) lililoandaliwa kwa ushirikiano baina ya United Nations Academic Impact ( UNAI) na ELS Educational Services, Inc.

Jumla ya wanafunzi 3,600 kutoka mataifa 165 walijitokeza kuwania shindano hilo ambalo hatimaye majaji waliwaibua wanafunzi 60 kutoka mataifa 36 kama washindi wa shindano hilo.

Amani Alfred Naburi ni mtanzania anayesoma Chuo Kikuu cha African Leadership University, huko Mauritius. Baadhi ya masharti ya kuingia shindano hilo lilitaka mshiriki lazima awe ni mwanafunzi aliye

Washindi hao 60 walipata fursa ya kusoma sehemu ya Insha yao mbele ya washindi wenzao na washiriki wengine waliokuwa wakihudhuria kongamano la vijana, katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mbali ya washindi hao 60 kuzungumza, wazungumzaji wakuu wengine walikuwa ni ambayo Rais wa Baraza Kuu Bw. Mogens Lykketoft na Bi Cristina Galach Naibu Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayesimamia idara ya Mawasiliano ya Umma ya Umoja wa Mataifa na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu kuhusi Vijana Bw. Ahmad Alhendawi aliwasilisha Salamu za Katibu Mkuu Ban Ki Moon.

Washindani wa Insha hiyo walitakiwa kuandisha Insha juu ya namna watakavyochangia katika utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( Agenda (2030). Ambapo kila moja wapo alitakiwa kuiandika insha hiyo yenye maneno yasiyozidi 2,000 kwa lugha nje ya lugha yake ya asili ya nchi anayotoka.

Tafsri yake ni kuwa walitakiwa kuandika kwa lugha sita ambazo ni rasmi na zinazotambuliwa na kutumika na Umoja wa Mataifa. Lugha hizo ni Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kichina, Kispanishi na Kirusi

Malengo waliyopewa washindani hao kuyandikia maoni hayo ni lengo namba kumi na mbili linalozungumzia Matumizi na Uzalishaji Bora ( Ensure Sustainable consumption and production ) lililowasilishwa kwa lugha ya Kifaransa, lengo namba kumi na sita ambalo linazungumzia kuhusu Amani, Haki na Taasisi Imara ( Promote just, peaceful and inclusive societies) lilowasilishwa kwa Kirusi, lengo namba kumi na tano linaluhusu Uhai juu ya Ardhi( Sustainably manage forests, combat desertification, halt and reverse land degradation, halt biodiversity loss ) lilowasilishwa kwa Kispanishi

Malengo mengine ni lengo namba kumi na tatu kuhusu kuchukua hatua kwa mbadiliko ya Tabia nchi na athari zake ( Take urgent action to combat climate change and its impacts), lengo namba tisa kuhusu Viwanda, Ubunifu na Miundo Mbinu ( Build resilient infrastructure, promote sustainable industrialization and foster innovation), lengo namba kumi na moja kuhusu kuifanya miji kuwa jumuishi, salama, na endelevu ( make cities Inclusive, safe, resilient and sustainable). Lengo hilo ndilo ambalo Mwanafunzi Amani Naburi aliliandika insha kwa lugha ya kiingereza kiasi cha kukoga nyonyo za majaj.

Lengo kuu la uandishi wa insha kwa lugha sita rasmi zinazotumika katika umoja wa Mataifa ni pamona na mambo mengine, kuwawezesha wanafunzi kujifunza lugha na tamaduni za nchi nyingine , kupanua wigo na fursa ya kujifunza mambo na changamoto zinazoikabili dunia na kujaribu kutoa mawazo yao yatakayoweza kusaidia katika kuzikabili changamoto hizo.

Lengo jingine ni kuwawezesha wanafunzi kutambua uwezo na vipaji vyao kama njia moja wapo ya kuwaandaa kuwa viongozi wa taifa la kesho.

No comments: