Advertisements

Wednesday, July 6, 2016

PISTORIUS AHUKUMIWA MIAKA 6 JELA

Mwanariadha mlemavu wa miguu wa Afrika Kusini
By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Mwanariadha mlemavu wa miguu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius leo amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp .

Kesi ya Mwanariadha huyo iliendelea kwenye mahakama kuu nchini humo na hukumu kutolewa muda mfupi uliopita.

Awali Pistorius alikuwa anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela baada ya vita ya kisheria iliyochukua takriban miaka mitatu.

Mwanariadha huyo Oscar Pistorius tayari ameshatumikia kifungo cha takribani miezi tisa jela katika kosa la awali wakati alipopatikana na hatia ya kuua bila kukusudia mwaka 2013.

No comments: