ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 1, 2016

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA RWANDA MH.PAUL KAGAME LEO.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mkewe Jeannette Kagame wakipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza  ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Rwanda Paul Kagame akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JINIA.


  Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Dkt. Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
 PICHA NA IKULU.

1 comment:

Anonymous said...

Mimi binafsi nimefurahi sana na Tendo la kuendelea Kujenga badala ya kubomoa...popote pale panapojitokeza Tofauti, ili kuimarisha Umoja wetu. Kanuni, "Ni Watu Wammoja". Hii itaimarisha mizizi ya "Umoja wa Afrika Mashariki", "Umoja wa Nchi Kusini mwa Afrika" na "Umoja Wa Afrika kwa ujumla".