Advertisements

Sunday, July 17, 2016

Reggae Time ya Pride FM.... July 16 2016.....VITA & UBAGUZI

Katika Reggae Time Jumamosi hii (Julai 16, 2016) tulijadili vita vinavyoathiri bara la Afrika. Unajua ni mataifa mangapi yako kwenye migogoro hivi sasa barani Afrika?
Unajua migogoro hiyo ni zaidi kuhusu nani na nani?
Unadhani mataifa ya nje yana nafasi gani katika kuchangia kuhusu vita hivi? Na ni kweli kwamba mataifa hayo yanastahili lawama kwa kinachoendelea barani mwetu?
Unaamini vita pekee iliyopo barani Afrika ni ya mauaji? Ya kiFikra je? Unaamini tunaweza kuishinda vita ya bunduki ikiwa tunashindwa ya kifikra?
WaAfrika walio nje ya nchi zao (Diaspora), wanakumbana na “vita” gani kwao na hata miongoni mwao?
Ungana nami na Rosslyn (mgeni wangu wiki hii) kuweza kusafiri kujadili haya kupitia muziki wa Reggae.
Kipindi cha REGGAE TIME kutoka Pride Fm Mtwara Tanzania hutayarishwa na kutangazwa na Mubelwa Bandio
Husikika kila Jumamosi kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki
Radio hii yasikika duniani kote kupitia tovuti www.878pridefm.com na kwa walio Marekani na Canada wanaweza kuisikiliza kwa kupiga namba 832 280 0658

No comments: