Advertisements

Friday, July 8, 2016

Sakata la Kessy lachukua sura mpya


Sweetbert Lukonge,

Dar es Salaam

Lile sakata la beki wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy kuhusu kukwama kwa uhamisho wake limechukua sura mpya ambapo sasa Chama cha Wachezaji Soka Tanzania (Suputanza) kinatarajiwa kukutana na wawakilishi wa Yanga na Simba ili kupata muafaka.
Hatua hiyo imefikiwa kwa kuwa tangu atue Yanga, ameshindwa kucheza kutokana na klabu yake ya zamani wa Simba, kutotoa barua ya kuidhinisha uhamisho wake.

Sputanza iliandika barua kwenda kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), likiomba mchezaji huyo kupata kibali, baada ya zoezi hilo kusuasua ndipo ukaomba kukutana na Simba na Yanga kwa nia ya kupata ufumbuzi.

Katibu Msaidizi wa Sputanza, Abeid Kasabalala ameliambia gazeti hili kuwa wamefikia hatua hiyo kutokana na pande hizo mbili kuonekana kutokuwa tayari kulimalizia suala hilo.

“Tunaendelea kupambana ili kuhakikisha Kessy anapata kibali ili aichezee Yanga katika michuano ya kimataifa. Tunasubiri majibu ya TFF lakini pia kesho Ijumaa (leo) tunatarajia kukutana na viongozi wa Simba na Yanga ili kulizungumzia suala hilo.

“Tumeshawasiliana nao na pande zote zimekubali hivyo tumuombe Mungu kwani viongozi wetu wa timu hizi mambo yao huwa wanayajua wao wenyewe mnaweza kukubaliana hivi baadaye wakabadilika,” alisema Kasabalala.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa pande hizo kukutana uso kwa uso kwa kuwa tangu sakata hilo lianze hakuna upande ulioonyesha kuwa tayari kukutana na mwingine.

Championi Ijumaa lilimtafuta Mayanja kupata ufafanuzi kuhusiana na hilo ambapo alisema:

“Kwa kifupi niseme tu mazungumzo yanaendelea vizuri, nimeona kuna nafasi nzuri ya kuendelea kubaki Simba ukizingatia niliishi na uongozi na mashabiki vizuri tu msimu uliopita ni vizuri ikieleweka hivyo kwa sasa.”

Alipotafutwa Katibu wa Simba, Patrick Kahemele kuzungumzia hilo, hakupatikana. Alipopigiwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe simu yake haikuwa hewani, upande wa Rais wa Simba, Evans Aveva yeye simu yake iliita bila ya kupokelewa

No comments: