ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 1, 2016

TANZANIA YAWA MWENYEJI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MASUALA YA USALAMA WA MTANDAO WA TEKNOLOJIA

Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklick (aliyeshika kipaza sauti) akijibu maswali mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle uliofanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt. Pembeni yake kushoto ni mgeni rasmi aliyefungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba pamoja na viongozi wengine. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklick (aliyeshika kipaza sauti) akiwasikiliza waandishi wa habari wakati wa mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle uliofanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt. Pembeni yake kushoto ni mgeni rasmi aliyefungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba pamoja na viongozi wengine.
 Washiriki waliohudhuria mkutano huo.
Mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle umefanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt ambapo wadau mbalimbali wa masuala ya teknolojia walikutana na kujadili matumizi salama ya mtandao.

Mambo makuu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ambao umefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba, ni usalama katika matumizi ya mitandao ya teknojia, Usimamizi wa utunzaji wa data na taarifa za siri na jinsi ya kukabiliana na hasara zinazotokana na matumizi mabaya ya mtandao yenye kuleta athari kwa watumiaji.

Imeeleza katika mkutano huo kuwa kila mwaka mabilioni ya dola hutumiwa na taasisi mbalimbali kujiweka salama na athari za kimtandao ambapo hata hivyo imeelezwa kuwa wezi wanaojinufaisha kupitia teknolojia kila kukicha wanabuni mbinu mpya za kufanya uharifu kupitia katika mitandao ikiwemo kuiba taarifa za siri kutoka kwenye makampuni na taasisi.

Taarifa zimebainisha kuwa hivi karibuni wizi wa kimtandao uliosababisha hasara ya dola za Kimarekani bilioni 300 umefanyika na kiasi cha dola bilioni100 umefanyika kupitia kadi maalumu za mihamala ya fedha na malipo, bara la Afrika likiwa moja ya wahanga wa wezi huu wa kimataifa.

Ripoti ya mwaka huu kutoka taasisi za Verizon kuhusiana na wizi wa kimtandao imebainisha kuwa kuwa wizi wa siri za makampuni ni wa pili kufanyika baada ya wizi wa fedha japo makampuni mengi hayajawa na mwamko wa kuwekeza katika kupambana na tatizo hili kubwa ambalo hivi sasa ni janga la kimataifa.

Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklicki amesema kuwa mikakati ya kuzuia wizi huu kuliko athari zinazojitokeza baada ya kuingiliwa katika mtandao na kuibiwa taarifa za siri za kampuni.

Alisema wizi huu wa kimtandao ni moja ya changamoto inayozikabili taasisi mbalimbali na makampuni ya biashara na ndio mwanzo wa kutengenezwa bidhaa bandia kwenye masoko na alisisitiza kuwa utunzaji wa taarifa za siri ni jambo la kwanza la msingi kwa kampuni

Mkutano huo ambao umedhaminiwa za taasisi za Oracle na CIO Afrika na kuhudhuriwa na watendaji kutoka serikali na taasisi mbalimbali umetoka na maazimio ya kuhakikisha uwekezaji wa kiteknolojia unafanyika katika kuhakikisha wizi huu wa kimtandao unadhibitiwa na makampuni kuwa makini kuhakikisha yanalinda taarifa zake za siri.

No comments: