ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 1, 2016

Chadema Kanda ya Kusini kufanya mikutano 8,764

By Haika Kimaro, Mwananchi;mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Mtwara. Viongozi wa Chadema Kanda ya Kusini wameunga mkono maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema ya kufanya mikutano 8,764 na maandamano kupinga kinachoelezwa ni udikteta nchini.

Kanda hiyo inayojumuisha mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mtwara imesema Operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Septemba Mosi inalenga kupinga viashiria vya udikteta vinavyoonyeshwa na serikali ya awamu ya tano.

Katibu wa Kanda hiyo, Philbert Ngatunga amesema maandalizi ya awali yameanza kufanyika na wanatarajia kila ngazi itafanya maandamano na mkutano mmoja na kufanya jumla ya jumla ya makundi ya maandamano na mikutano 8,764.

Ngatunga pia amelaani kauli ya msajili wa vyama vya siasa dhidi ya Chadema aliyoitoa kupitia vyombo vya habari Julai 27, kuwa mambo yote aliyoyasema hayapo.

Kauli hiyo inaunga mkono maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema katika kikao cha dharura cha Julai 23 hadi 26 mwaka huu.

1 comment:

Anonymous said...

Mikutano 8,764? Je watapata muda wa kufanya kazi?