Advertisements

Monday, August 15, 2016

JICHO LA LISSU KWA ABOUD JUMBE

Alikuwa pia mwasisi wa Muungano ulioizaa Tanzania miezi michache baadaye. Baada ya Sheikh Abedi Amani Karume kuuawa mwezi Aprili 1972, Jumbe aliteuliwa kuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, na alishikilia madaraka hayo hadi Januari 1984.

Wasomi wa Muungano wameandika kwamba, wakati Rais Karume anauawa, uhusiano wake na Mwalimu Julius Nyerere ulikuwa umeharibika kiasi kwamba Jumbe (kwa upande wa Zanzibar) na Bhoke Munanka (kwa upande wa Tanganyika) ndio walikuwa kiunganishi cha mawasiliano kati ya Mwalimu na Karume.

Hii pengine ndio sababu Mwalimu alitumia ushawishi wake kuhakikisha Jumbe anateuliwa kumrithi Karume.

Hata hivyo, Jumbe atakumbukwa zaidi na historia kwa upinzani wake kwa mfumo wa sasa wa Muungano kuliko, pengine, kwa jambo jingine lolote.

Jumbe alikuwa mwanasiasa wa kwanza, baada ya era ya (uongozi wa) Karume, kutambua kwamba muundo wa serikali mbili ulikuwa umeipokonya Zanzibar mamlaka yake na kuyahamishia Tanganyika.

Alikuwa wa kwanza kutambua kwamba, kuzaliwa kwa CCM katika context (mtazamo) ya Muungano, kulimaanisha mwisho wa mamlaka yaliyokuwa Zanzibar chini ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964.

Sio tu alitambua bali pia Jumbe alichukua hatua kupinga Zanzibar kupokonywa mamlaka yake hayo.

Ili kufanikisha azma yake, Jumbe alilazimika kumwachisha kazi Mwanasheria Mkuu wake aliyempewa na Mwalimu Nyerere, Damian Lubuva, na kumwajiri Bashir Ebassuah Kwaw Swanzy, Raia wa Ghana, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Kwaw Swanzy ndiye aliyeandaa ‘hati ya mashtaka’ dhidi ya Muungano iliyokamatwa na watu wa usalama wa Mwalimu na baadaye kutumika kumsulubu Jumbe kwenye kikao cha NEC ya CCM Dodoma Januari 1984. Kwa sababu ya upinzani huo, Jumbe aling’olewa madarakani pamoja na Waziri Kiongozi wake Ramadhani Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Kwaw Swanzy alitangazwa kufukuzwa nchini.

Mwalimu akatangaza ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa’ Zanzibar na Wazanzibari wengi wapinzani wa Muungano, kama Mwanasheria Mkuu wa kwanza Wolfgang Dourado, kuwekwa kizuizini.

Miaka 10 baada ya kuondolewa madarakani, Alhaj Aboud Jumbe alichapisha kitabu chake juu ya Muungano, ‘Miaka Thelathini ya Dhoruba’, ambako aliweka bayana ugomvi wake na Mwalimu juu ya Muungano.

Jumbe ni kiongozi pekee wa juu wa rika la wapigania uhuru wa Tanzania kuandika memoirs zake juu ya Tanzania na matatizo ya Muungano wake.

Hata Mwalimu hakufanya hivyo na alikufa na siri zake juu ya mambo mengi makubwa yalitokea wakati wa utawala wake.

Kwangu mimi, hii ndio merit (faida) kubwa na mchango mkubwa wa Alhaj Aboud Jumbe kwa kizazi cha sasa na vijavyo Tanzania.

Alikuwa na ujasiri wa kusema na kuandika juu ya ‘The Forbidden Subject’, tena katika kipindi cha Mwalimu Nyerere ambapo ujasiri wa aina hiyo ulikuwa ni jambo la hatari kubwa.

Kwa sababu hiyo hiyo, Jumbe alilazimika kuishi theluthi ya mwisho ya maisha yake ‘kifungoni’ Mji Mwema, Kigamboni, ambako alipelekwa mara baada ya kung’olewa madarakani mwaka ’84.

Sikuwahi kubahatika kuonana na Alhaj Aboud Jumbe wakati wa uhai wake. Hata hivyo, nimejifunza mengi sana kutoka kwake, hasa ujasiri wa kuuhoji Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Jumbe amekuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye mjadala wa Muungano kwa zaidi ya miongo mitatu sasa.

Ninadiriki kusema kwamba, hoja ya Serikali Tatu ilianzia kwa Jumbe. Roho yake ilikuwa kila mahali wakati wa mchakato wa Katiba Mpya kati ya 2011 na 2014.

Kivuli chake kilikuwa kila mahali wakati wa Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014. Pengine kuliko hata Mwalimu Nyerere, Jumbe ndiye aliyetufundisha kuufahamu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Atakumbukwa kama mmoja wa waTanzania maarufu na wapigania uhuru wakubwa wa Zanzibar ya baada ya Muungano.

Adieu Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi. Adieu Mtanzania jasiri. Adieu shujaa wa uhuru wa Zanzibar.

MWANAHALISI

4 comments:

Anonymous said...

Lissu and heresay; inseparable! This guy is a lawyer? Unbelievable!

Anonymous said...

The article's author is entitled to his own opinion. There are many Tanzanians who have different viewpoint. Like many Zanzibaris who immigrated from Tanganyika, the late Mh. Jumbe embraced the mainland as his home on the same par as his adopted land of Zanzibar. He had no viable reasons to hate his original roots, as the author has characterized. R.I.P our mainland son.

Anonymous said...

Jicho la Lisu kwa hayati Aboud Jumbe ni sawa na jicho la mwanga kutoka katika kundi la wanga anaetaka kujifanya mganga kwa mtoto waliemwaangia. Kweli kabisa muheshimiwa Jumbe alikuwa muumini wa Serikali tatu japo baadhi ya tetesi zilisema Jumbe alinogewa na madaraka ya uraisi kiasi kwamba ilifikia hatua ya kuwa na nia ya kujitangaza kuwa yeye ni raisi wa maisha au mfalme wa visiwa hivyo vya Zanzibar. Lakini azma yake ya kuwa raisi wa maisha au mfalme wa wa visiwa vya Zanzibar isingetimia kama Zanzibar itakuwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa ili kujaribu kutimimiza azma yake hiyo ya kuwa mfalme wa Zanzibar ndipo muheshimiwa Aboud Jumbe alipoanza mikakati ya kuuchokonoa Muungano na tetesi zinaeleza lengo hasa ilikuwa kuiondoa Zanzibar katika muungano moja kwa moja hilo la Serikali tatu ilikuwa ni kama kipeleka uposa au kifunga maghari,hizo ni tetesi Mungu ndie mwenye kujua zaidi. Lakini la uhakika wakati muheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi akiandaa mikakati yake hiyo ya kudai serikali tatu katika Muungano wa Tanzania dili lake likaja likavuja katika mazingira ya kushangaza na kutatanisha kwani hata wazanzibari wengi tulushindwa kufahamu muheshimiwa raisi wakati huo alihusika na kosa gani la uhaini isipokuwa tulielezwa raisi na baadhi ya viongozi wake wa karibu hasa wale vigogo wa "MBM" wanashikiliwa kwa kosa la uhaini na raisi kaamriwa kujiuzulu. Vipi dili la muheshimiwa Aboud Jumbe la kudai serikali tatu au kuvunja muungano livuje na habari zimfikie Mwalimu Nyerere wakati ilikuwa siri ya wazanzibari na mipango yote ilikuwa ikisukwa Zanzibar? Jibu ni kwamba dili hilo lilivuja kwa sababu ya unafiki wa wazanzibari wenyewe na kinara wa unafiki katika wanafiki hao ni Seif Sharif Hamadi. Seif Sharif ndie aliepuruchuka na kwenda kwa Mwalimu Nyerere kutoboa siri ya mipango ya Aboud Jumbe Mwinyi juu ya azma yake ya kudai serikali tatu. Na mashuhuda waliomshudia Seif Sharif wakati anapeleka madai yake mbele ya Mwalimu Nyerere wanasimulia yakwamba Seif Sharif alikuwa akilia kwa Majonzi,tena kilio cha kwikwi ambacho mara nyingi kumnyamazisha mtu aache kulia kunakuwa kuna kazi kweli kweli. Sasa huu upuuzi aliouandika Tundu Lisu hapo juu wa kupotosha umma mimi nikisika kaingia matatizoni na serikali ya Tanzania kwa kuzungumza uongo wala sitoshangaa maana inaonekana huyu Lisu hizi drama za kipuuzi na serikali anazipenda lakini nnaamini ukaribu wa Lisu wa kwenda kutumia muda wake Jela upo karibu sana na haitakuwa kwa sababu yeye ni shujaa bali ni ujinga wake. Seif Sharif ahai na pengine anapitia mitandaoni kama si yeye basi wapambe wake watakuwa wanasoma wanaweza kumfikishia habari yakwamba yeye ndio chanzo cha mueshimiwa Aboud Jumbe na baadhi ya viongozi wake kuamriwa kujiuzulu na kuweka mahubusu kwa muda usiojulikana kwa azma yao ya kudai muungano wa serikali tatu Zanzibar na kama yeye Seif Sharif ni muislamu wa kweli anaeamini yakwenda kumkuta muheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi mbele ya Mungu katika hali ya majonzi kwa kumsaliti na akatae yakuwa hakufanya hivyo au atubu kwa kuacha kuendeleza fitna Zanzibar hadi kuwapelekesha wazanzibari baada ya kuabudu Mungu wa haki wana abudu siasa hivi sasa kwa kususiana hadi misikiti ya kusalia. Kwa hivyo Seif,Lisu wote ni wanafiki wakubwa sema Lisu hajui anachokiongea aidha anafanya hivyo kwa makusudi kwa nia ya kupotosha umma au mgonjwa wa akili kwa kifupi wote ni wanga wanaojaribu kujifanya waganga katika siasa za Zanzibar.

Anonymous said...

inasikitisha sana zanzibar miaka hamsini ya uhuru hakijulikani kinachopiganiwa wala kutetewa, ni vurugu tu. wengi wa wanasiasa wa kizanzibari wana agenda zilizo wazi na zilizojificha.agenda kubwa zaidi ya zote ni mapenzi ya madaraka na maguvu ya kiutawala. wanasiasa wetu watatetea, watapigania mambo ambayo yatawasaidia kupata nguvu za madaraka, lakini wanakuwa wakali kama mbwa mwitu kuyageuka yale waliyoyatetea jana tu kama wakiona lengo lao halina uwezekano wa kufikiwa. marehemu Karume wakati wa kujadili na kutia saini mkataba wa muungano alimpa mwanasheria wake mkuu Dorado likizo ili asilete pingamizi alisaini mkataba huo bila kujipa wakati wa kutosha kuujadili na kuupitia mkataba huo walau kwa mashauriano na wenzake, aliunganisha tu mradi muungano ungemlinda asipinduliwe na maadui wa mapinduzi. Jumbe aliutetea muungano kwa nguvu zote na hata kuamua kuua Afro-Shiraz na TANU ili kuimarisha muungano. lakini alipoona ndoto yake ya kuwa rais wa jamhuri ya Tanzania haina mwelekeo wa kutimia na kikwazo kikubwa kikiwa ni Nyerere akaamua kuwa mbogo. Seif Sharif aliamua kumtosa Jumbe kwa kumsaliti kwa Nyerere akijua zawadi nono ya urais wa Zanzibar ndio angetunukiwa na Nyerere. alifanya usaliti huo huku akijua fika alichokuwa anakipigania Jumbe cha serikali tatu naye anakiamini. Lakini alipouona mwanya wa madaraka ya urais wa Zanzibar ambao ndio ndoto yake ya kufa na kupona itaweza kutimia hata kama kwa kumsaliti Mzanzibar ambaye alimsaidia kwa yote mema kama alivyoeleza yeye mwenyewe aliitumia tu nafasi hiyo bila kujali athari za baadae. sawa, kwa usaliti huo mzee wa Butiama akampa zawadi wa uwaziri kiongozi. nasikitika baadae kila anayekuwa kikwazo cha Seif kuupata urais atampiga vita hata kama kwa atomic. siasa za Zanzibar kwa miongo mitatu zimekuwa za ajabu ajabu Unguja kuna staili tofauti na Pemba kisiasa. wazanzibari unafiki umetuandama ndio damu yetu na ndio pumzi yetu. nathubutu kusema wengi wetu hatujui tunachokitaka, wanasiasa wanatuchanganya-confuse tu siasa inatumaliza visiwani hakuna liendalo furaha imeondoka, maendeleo ni nightmare. alinichekesha sana Amani Karume mara baada ya kumaliza kipindi cha miaka kumi ya urais ndipo akaanza kuidai hati halisi ya muungano-article of the union. nathubutu kusema wazanzibari hatuna wanasiasa werevu na wakweli- WE LACK SMART AND TRUSTFUL POLITICIANS Unafiki tu!!Tusubiri nusra ya Mwenye Enzi Mungu.