ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 1, 2016

JPM HAKUNA MCHANGA UTAKAOSAFISHWA NJE YA NCHI TOKA MIGODINI

RAIS John Pombe Magufuli Amesema hakuna mchanga wowote wa madini kwenda nje ya nchini 
Moja wa mgodi wa Dhahabu huliopo wilayani kahama wa Buzwagi kati ya migodi inayosafirisha mchanga nje ya nchi ambapo Rais magufuli amepinga Marufu kusafirisha mchanga huo 
Mitambo ya kuchimba dhahabu katika mgodi wa buzwagi ambapo uchimbwa kwa dhahabu hiyo na baadhi ya mchanga wenye madini kusafirishwa nje ya nchi kwa utalamu zaidi 
Moja ya Dapa la kubeba mawe ya dhahabu na madini mengine baada ya kuchambuliwa katika mgodi huu uliopo wilayani kahama 
Eneo moja wapo la shimo la mchanga wa dhahabu 
Moja ya Madapa Makubwa yakiwa katika hatua ya kupakia mchanga au mawe yenye dhahabu katika mgodi wa dhahabu 
Dapa kubwa linyeuwezo wa kupakia tani 200 za mawe ya dhahabu katika mgodi wa dhahabu wilayani kahama 
Baadhi ya Maroli yakiwa yamembeba Makotena ya mchanga wa madini mengine toka mgodi wa dhahabu wa buzwagi Acaci yakiwa yanaelekea jiji dar kwa kusafirisha nje ya nchi
baadhi ya maroli ya mchanga toka mgodi wa buzwagi kuelekea jiji dar kwa kupelekwa nje ya nchini. 

MOHAB MATUKIO

4 comments:

Anonymous said...

Safi sana Mhe Rais,nadhani ndani ya huo mchanga pia tulikuwa tunaibiwa huku tukiambiwa ni mchanga,tunakuombea Rais wetu Mungu azidi kukulinda na wabaya

Anonymous said...

Mheshimiwa kwani huu sio mkataba walioingia maRais wa awamu 2 zilizopita. Kwa msingi huo.unakatisha mkataba bila.kujadili na hao wamiliki. Pili je umeanzisha kiwanda cha kukobolea huo.mchanga kuweza kupata mali halisi hapa nchini. Wao wanaupeleka nje kwa maana wana kiwanda. Na tunachobakia nacho sisi ni mabakia sawa na makombo tu.
Nakuomba mheshimiwa Rais kaa na washauri na wanaofanya kazi hiyo.kupata jibu la ni asilimia ngapi Tanzania au wana Bulyankulu wanapata hapo. Sivyo tutaendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu. Anzisha Viwanda jambo ambalo ni.mtihani pia. Piga hesabu ngombe, mbuzi, Kondoo, ukiacha kuku na nguruwe wangapi wanachinjwa nchini kwa siku, juma mwezi na zinaenda wapi. Matunda yanaozea sokoni Bakhresa pekee anaiweza kazi. Tanzania hiyo baba JPM.nenda nayo taratibu. Walipita wengi bila mafanikio. Pata ushauri.

Anonymous said...

Safi sana kama hao wanaosafirisha mchanga nje ya nchi yetu wana nia njema na nchi yetu kwanini hiyo mitambo ya kuchuja huo mchanga wasiejenge kwetu tukaona laivu wanachokipata. Vile vile tungeweza kutengeneza ajira kwa watu wetu. Kamwe tusikubali Tanzania kuwa shamba la bibi kwa walowezi kutoka nje.

Anonymous said...

Waliokuibia ni wale walio saini mkataba upate 4% na wao wachukue 96%.
Huo mchanga si lolote si chochote.
Hiyo serikali ya wakurupukaji isubiri tu kushtakiwa kwa kuvunja mkataba.