Advertisements

Thursday, August 4, 2016

KITILYA NA WENZAKE WAPINGA KUNYIMWA DHAMANA

Kamishna Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Mapato
By James Magai, Mwananchi jmagai@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Washtakiwa watatu akiwamo aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya wanaokabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha katika kesi mbili tofauti wamefungua kesi ya kikatiba wakipinga kunyimwa dhamana.

Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomon, wanaoshtakiwa katika kesi moja na nyingine ya utakatishaji fedha inayomjumuisha, Gidion Wasongo wamefungua kesi hiyo Mahakama Kuu.

Mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wa pili ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Mashtaka ( DPP).

Kesi hiyo ya kikatiba namba 14 ya mwaka 2016, Kitilya na wenzake wanapinga kifungu cha 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kinachozuia dhamana kwa mashtaka ya utakatishaji fedha.

No comments: