Advertisements

Saturday, August 6, 2016

Makonda apiga marufuku Ukuta, awapa meno FFU


By Tumaini Msowoya, Mwananchi tmsowoya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapa rungu askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani hapa kuwadhibiti watakaothubutu kufanya maandamano ya kuunga mkono operesheni ya Chadema iliyopewa jina la Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta).

Chadema walizindua operesheni hiyo na kutoa maazimio matatu ambayo yatatekelezwa nchi nzima ikiwamo mikutano ya hadhara ambayo itafanyika Septemba Mosi, mwaka huu.

Wanadai wanataka kuzuia matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini inayofanywa na Rais, John Magufuli. Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kukitembelea kikosi cha FFU Ukonga jana, Makonda aliwataka askari wajipange kudhibiti Ukuta na hawana haja ya kusubiri maagizo kutoka kwa kiongozi yeyote.

1 comment:

Anonymous said...

makonda punguza show za kwenye vyombo vya habari badala yake fanya kazi kwa manufaa ya jiji na wakazi wake.!!