Advertisements

Monday, August 22, 2016

USHAURI WAKO NI MUHIMU SANA MAANA UNAWEZA KUNISAIDIA JUU YA HATIMA YA MAISHA YANGU

Binafsi ninaomba kuelezea story yangu (Ndefu) kuhusu hisia za kishoga.
Nimekuwa katika familia yenye maadili ya kikristo nikiamini kuwa ngono ni dhambi.
Nimekuwa na ratiba ya kusali, ratiba ya kusoma hadi nikahitimu kidato cha sita bila kuhangaika na wasichana na walipojaribu kunifuata fuata niliamua kuwatolea nje.
Mara nyingi nilipokuwa najiona mtupu bila nguo nilifurahia mwili wangu mwenyewe na kujikuta jongoo akipanda mtungi.

Nikiwa chuo kikuu pia niliendelea kuwa mtu wa Mungu mara nyingi nikiwa karibu na watumishi wa Mungu na kuhubiri neno la Mungu chuoni. Ghafla nikajisikia KUVUTIWA sana na rafiki yangu wa kiume. Sikujua ninataka nini kwake ila akiwa hayupo chuoni nilikuwa sijisikii furaha kama akiwa karibu na mimi. Nilianza kujishangaa maana sikuwahi kuvutiwa na wasichana. Inakuwaje navutiwa na mwanaume mwenzangu? Niligundua napenda umbo lake, lips zake na hata macho yake. Lakini ni mwanaume mwenzangu!! Kutokana na ratiba ya masomo na imani yangu pia nilifanikiwa kumaliza chuo bila kuonyesha udhaifu wowote kuwa nina hisia za kimapenzi kwa mwanaume mwenzangu.

Baada ya kumaliza chuo niliajiriwa kwenye kampuni ikanilazimu kuishi ghetto. Hapa ndipo nilipokaa na kutathmini hisia zangu maana nilikuwa na muda wangu mwenyewe. Niligundua kuwa mwanamke aliye mtupu hanivutii kabisa ila mwanaume aliye kama alivyozaliwa ananivutia sana!! Sikujua nifanye nini zaidi ya kumwomba Mungu. Nilienda kwenye maombi mbali mbali bila mafanikio. Nilikutana na vijana wenzangu mara nyingi baadhi yao walinivutia sana na hata kutamani kufanya nao romance; ila hofu ya Mungu ilinikataza hata nilipogundua kuwa mwingine ana hisia kama za kwangu.

Mwaka jana mwishoni nikakutana na rafiki ambaye tumekuwa kama ndugu wa kuzaliwa kwa jinsi anavyonijali na ninavyomjali; lakini moyoni mwangu nimekuwa nikivutiwa mno na hisia za kimapenzi juu yake. Mwaka huu akapata mchumba ndipo ikawa uchungu mkubwa kwangu na kugundua kuwa hisia zangu juu ya mwanaume mwenzangu ni kubwa mno. Nikajaribu kujibadilisha naku date na mwanamke mmoja ambaye alikuja ghetto na kutaka tufanye mapenzi; ila ghafla sikuvutiwa nae kabisa tulipoanza tu kumtomasa sikuweza kuendelea maana sikupata hisia zozote, akakasirika na kuondoka.

Kwa sasa niko njiapanda ya maisha yangu. Sijitambui na hata nikienda kanisani ombi langu ni Mungu aniondolee hisia hizi lakini nikigeuka nakutana na wanaume wanaonivutia na sio wanawake wanaonivutia. Wakati mwingine nikitafakari naona kabisa natamani kuishi na mwanaume ila sio kufanya tu mapenzi ila hata tu kusaidiana katika maisha na kufanya romance, Upande mwingine jamii inayonizunguka inaniheshimu sana na kutambua mchango wangu kwao ila wananihimiza kutafuta mwanamke wa kuoa; Nitatafutaje mwanamke wakati sina hisia juu yao? Wazazi na ndugu wengine wananishauri niwe makini na wanawake na nijitahidi kuoa mapema ili nianze kulea watoto kwa kuwa kama ni kipato ninacho na kama ni elimu ninayo. Natamani ningeweza kuondoka duniani bila kufa!

Maji yamenifika shingoni maana sina hata chembe ya hisia kwa wanawake.

(Note: Mimi ni mwanaume lijali na pia ninapata night dreams ila hata nikiota nafanya ngono naota nikifanya matomaso tu na mwanaume!)

USHAURI WAKO NI MUHIMU SANA MAANA UNAWEZA KUNISAIDIA JUU YA HATIMA YA MAISHA YANGU

No comments: