Advertisements

Monday, August 15, 2016

WANANCHI WA KATA YA MWENDAKULIMA WALALAMIKA KUTOSHIRIKISHWA MAKABIDHIANO YA SHULE NA MGODI WA BUZWAGI

Moja ya Darasa ambalo ilimejengwa kwa msaanda wa mgodi wa buzwagi huku nguvu za wananchi zikiwa zimetupiliwa mbali kama jinsi matofari 2300 ambyo wanakijiji wa Budushi walinunua kwa fedha zao. 
Two in one nyumba za walimu mpya katika shule ya msingi Budushi 
Vyoo vya shule ya msingi Budushi ambapo kuna matundu 32 kwa wavulana na wasichana 
Moja ya jengo la Madarasa ya shule ya msingi Budushi kata ya mwendakulima kati 
Mbunge wa jimbo la kahama Jumanne kishimba akiwa na Afisa Elimu wa shule za msingi Aluko Lukolela Mwenye kitabu cha blue wakisubiri ufunguzi wa shule hiyo toka katika uongozi wa mgodi wa buzwagi 
Mafundi wakikamilisha ufungwaji wa madirisha katika baadhi ya madarasa katika shule hiyo ya Budushi 
Eng. Asa Mwaipopo pia ni meneja wa mgodi wa Buzwagi akitolea maelezo juu ya ujenzi wa shule hiyo kwa mkuu wa wilaya ya kahama Fadhili Nkurlu katika kijiji cha Budushi wilayani kahama mwenye kofia nyeupe ni mkuu wa wilaya ya kahama 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa kahama Abel shija wakiangalia ujenzi wa shule hiyo 
Mkuu wa wilaya ya kahama Fadhiri Nkurlu na Mbunge wa jimbo la kahama mwenye upara nyuma ya Dc jumanne kishimba kuli ni kaimu kurungezi wa mji 
Eng. Asa mwaipopo akimuonyesha mkuu wa wilaya ya kahama Fadhili Nkurlu moja ya madarasa mwenye miwani na kofia nyeupe 

Mkuu wa wilaya ya kahama Fadhili Nkurlu Akinywa maji salama katika kisima kilichojengwa na mgodi huo wa buzwagi katika shule ya msingi Budushi 
KAHAMA


Baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Budushi kata ya Mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameulalamikia Mgodi wa Madini wa Acacia Buzwagi kwa kufanya mambo kijijini humo bila kuwashirikisha wananchi,ambao walianzisha ujenzi huo.

Akizungumza kabla ya zoezi la kukabidhiana Shule ya Msingi Budushi yenye vyumba 6 vya madarasa, ofisi mbili na nyumba moja ya walimu, Mtendaji wa Mtaa wa Mwendakulma Kati Christopher Laurent amesema mradi huo uliibuliwa na wananchi wenyewe na kuanza hatua za ujenzi kabla ya kupata ufadhili kutoka mgodi wa Buzwagi.

Alisema tangu mgodi huo ufadhili ujenzi wa shule hiyo wananchi wamekuwa hawashirikishwi katika shughuli za ujenzi huo jambo ambalo ni kuwatenga waanzilishi wa mradi huo kutokana na wanafunzi wa kijiji hicho kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata Elimu vijiji jirani.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwendakulima Kati Abdulrahman Abdallah baada ya wananchi kuanzisha mradi huo kisha kufadhiliwa na Mgodi wa Acacia Buzwagi lakini Halmashauri ya Mji wa Kahama haijachangia chochote ili kuwaunga mkono wananchi walioanzisha ujenzi huo.

MOHAB MATUKIO

No comments: