Advertisements

Wednesday, September 7, 2016

ADAKWA AKIUZA WASICHANA KAMA NJUGU

Image result for MAHAKAMA
By Florence Focus, Mwananchi mwannachipapaers@mwananchi.co. tz

Musoma. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Julita Lucas (30), mkazi wa kijiji cha Masinki Wilaya ya Serengeti kwa tuhuma za kufanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu anaowauza kuanzia Sh150,000 hadi Sh300,000.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Ng’anzi amesema Septemba 3, saa 9.00 alasiri, Lucas alikutwa akiwa na wasichana watano (majina yamehifadhiwa) aliokuwa amewaficha nyumbani kwake kwa lengo la kuwauza na wengine kuwaozesha kwa wanaume wenye kuhitaji.

Amesema baada ya mama huyo kuhojiwa alikiri kufanya biashara ya kuuza wasichana kwa bei ya kati ya Sh 150,000 hadi 300,000, kwa kuangalia ukubwa wa umbo na siyo umri.

“Baada ya kufanya mahojiano na wasichana hao wenye umri kati ya miaka 15 hadi 28, walisema wametokea katika kijiji cha Muhejangila Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera,” amesema.

Kamanda Ng’anzi amesema polisi wanaendelea na uchunguzi dhidi ya mama huyo, ili kubaini mtandao wa biashara hiyo haramu ya binadamu.

“Tunaendelea kumuhoji, tunataka kujua iwapo kituo cha mwisho cha biashara hiyo ni hapa ndani tu au ni hadi nje ya nchi , biashara hiyo ilianza lini na idadi ya wasichana waliokwisha uzwa na waliuzwa wapi,”

Kamanda Ng’anzi alisema baada ya upelelezi kukamilika, mama huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

1 comment:

Anonymous said...

Hah! Ameshakubali kuwa anafanya biashara hiyo na jwa bei hii. Sidhani kama ni swala la kuchukua muda wa upelelezi. Mara moja aandikishe mlolongo wa mpangilio wa hao aliokutwa nao alipangilia kuwauza wapi na kama alishawapata wanunuzi awataje. Asema kashauza wapi na wangapi. Ndani ya siku tano taarifa ziko na kukamilisha shitaka sio mwezi mzima. Awekwe mchunguzi stadi na mkakamavu tuache longolongo zitazoleta hongo kwani hela anayo!