Advertisements

Tuesday, September 6, 2016

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA AMKARIBISHA MREMA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema wakati alipomtembelea ofini kwake ili kujua matatizo mbalimbali yanayoikabili bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Jeshi la Magereza (aliyesimama kushoto) akisoma taarifa ya utekelezaji wa sheria ya bodi ya parole kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema (wa kwanza kulia) wakati Mwenyekiti wa Bodi alipomtembelea Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja (katikati) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Magereza (hawapo pichani) wakati alipomtembelea Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja (kushoto)ili kujua matatizo mbalimbali yanayoikabili bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema wakati alipomtembelea ofisini kwake ili kujua matatizo mbalimbali yanayoikabili bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja pamoja na baadhi ya maafisa ya hilo wakati Dkt. Mrema alipokwenda kumtembelea ili kujua matatizo mbalimbali yanayoikabili bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akiagana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja wakati Dkt. Mrema alipomtembelea ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.

No comments: