Advertisements

Friday, September 16, 2016

DC AHIMIZA KUANZA KWA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARI

Image result for wilaya ya tanganyika
Na Mussa Mbeho,Katavi.
WAKAZI wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wameombwa kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji na kata katika kuweka mikakati ya kuanza kwa ujenzi wa shule za Sekondari kwa kila kata ,ili kuweza kuinua kiwango cha elimu katika wilaya hiyo.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando,wakati akizungumza na wananchi kwenye mikutano ya Hadhara uliofanyika katika kata za Ilangu na Bulamata wilayni humo.

Mhando amesema kuwa umefika wakati wa kushirikiana kati serikali na wananchi kwa kukutana pamoja na kujadili mipango ya kuanza kwa ujenzi wa shule za sekondari kwenye kila kata ili kuweza kupunguza changamoto zanazowakabili wanafunzi katika wilaya hiyo.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ametoa onyo kali kwa wazazi na walezi wote watakaohusika na kuwaozesha watoto wa shule huku akisema kuwa mwanaume atakayeoa au kumpa ujauzito mwanafunzi atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungwa miaka 30 bila huruma.

Nae Afisa Mtendaji wa Kata ya Bulamata Bw.Godfrey Mbalazi,akisoma taarifa ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Bulamata inayojengwa katika kijiji cah Busongola amesema tayari wamekusanya zaidi ya shilingi milioni 12 kwa kuanza na ujenzi wa shule hiyo.

Wakati huo huo,Mkuu wa Wilaya akiwa katika Shule ya Msingi Isubangala iliyopokata ya Ilangu amezindua vyumba 3 vya madarasa na ofisi moja ambavyo vimefikia usawa wa renta katika ujenzi ambapo shule hiyo iliyoanzishwa 17.1.1980 mpaka sasa ina wanafunzi 1071.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ameruhusu kufanyika mikutano ya viongozi wa vijiji na kata ilivyokuwa imezuiliwa na uongozi wa makazi ya mishamo kutokana na mgogoro wa kiutawala.

Katakika taarifa yake Afisa Mtendaji wa kata ya Ilangu Bw.Seuri Mishileki amesema,mikutano ilikuwa imezuiliwa kwa takribani wiki mbili mpaka sasa ambapo ameeleza shughuli nyingi za maendeleo kukwama kutokana na kutokuwepo kwa mikutano inayowakutanisha viongozi na wananchi.

Chanzo cha Mvutano ni baada ya mwenyekiti wa kijiji cha Ilangu kujiudhuru na kuvutana kuwa anayechukua nafasi atoke makazi ya mishamo au upande

No comments: