Advertisements

Monday, September 19, 2016

DC:TUTAWAONDOA WALIOJENGA KARIBU NA VYANZO VYA MAJI

Mussa Mbeho na Issack Gerald,Katavi

MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Bw.Salehe Mbwana Mhando,amewataka wakazi wote wa wilaya hiyo waliovamia katika maeneo ya vyanzo vya maji kuondoka wenyewe kabla ya Oparesheni ya kuwaondoa kwa nguvu haijafika katika maeneo hayo.

Kauli hiyo imetolewa jana na mkuu huyo wa wilaya wakati akaizungumza na wananchi wa kitongoji cha Luhafe kilichopo katika kijiji chavikonge kata ya majalila katika mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha na kukagua maeneo ya vyanzo vya maji wilayani humo .

Bwana Mhando amesema kuwa tangu mwanzo wa ziara yake wilayani humo amekutana na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali unaofanywa na baadhi ya wananchi ambao wamevamia maeneo hayo na kujenga makazi jambo ambalo linapelekea vyanzo hivyo kukauka .

Alisema kutokana na hali hiyo wananchi wote waliojenga kwenye vyanzo hivyo waondoke haraka iwezekanavyo kabla serikali ya wilaya hiyo haijachukua hatua za kuwaondoa kwa nguvu ifiikapo mwezi oktoba mwaka huu.

“Ngugu zangu mliopo karibu na vyanzo vya maji mimi natoa wiki mbili muwe mmeondoka wenyewe katika maeneo hayo kabla hatujaja kuwaondoka kwa nguvu na kama hamtaondoka basi mwezi oktoba tutakuja kuwaondoka sisi wenyewe”Alisema mhando.

Aidha Bwana Mhando amesema eneo ambalo wananchi wanatakiwa kuondoka ni eneo la kamama ,misanga,bariadi ,Ijamba,Western , Misanga na palipo na mto Sabaga ambapo kuna vyanzo vya maji huku akiwataka wananchi wa maeneo hayo kuhamia katika kitongoji cha Luhafe .

Wakati huo huo mkuu huyo wa wilaya amekitangaza rasmi kitongoji cha Luhafe kilichopo kijiji cha Vikonge kata ya Majalila,kuwa ni eneo halali la makazi ya wananchi pamoja na shughuli za kibiashara baada ya kumalizika kwa mgogoro wa uhalali wa eneo hilo ulikuwa umedumu kwa muda mrefu.

Nae Afisa Mipango miji na Vijiji katika Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Elisha Mengele,ametoa wito kwa uongozi wa kitongoji hicho kuendesha sense ya kubaini idadadi ya watu ili waanze kupimiwa viwanja kwa ajiri ya kujenga makazi ya kudumu .

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa ambao wanaishi katika maeneo hayo wamesema kuwa wao wako tayari kuondoka huku wakiripokea kwa furaha tangazo la mkuu huyo wa wilaya na kuahidi kuwa kilichobaki sasa ni kufanya kazi kwa bidii ili kuweze kujileta maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe mhando mwenye koti jeusi pichani akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Luhafe baada ya kutembelea kitongoji hicho jana(picha na mussa mbeho).

No comments: