Advertisements

Friday, September 2, 2016

FIFA YATOA MFUMO MPYA KWA MAMENEJA WA USAJILI WA WACHEZAJI

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetoa taarifa kwa mameneja wote wa usajili kwa mfumo wa mtandao (TMS-Transfer Matching System Managers) wanaotakiwa kujiunga kwenye mfumo mpya wa mawasiliano wa GPX kwa ajili ya kupata taarifa zaidi za wachezaji.

Mfumo huo unatarajiwa kurahisisha usajili wa mchezaji mmoja kwenda timu nyingine lakini pia unatarajiwa kusaidia kupata taarifa kamili za mchezaji husika na kurahisisha mawasiliano ya TMS Managers ya nchi nzima.
Global Players Exchange (GPX) ni mtandao wa kawaida kama ilivyokuwa mitandao mingine ya kijamii ambapo kwa kutumia mfumo huu utasaidia kuwa na mawasiliano ya karibu na Fifa kwa kuwa utakuwa umeunganishwa dunia nzima.
Mfumo huu kwa Tanzania utawahusisha mameneja wa timu za ligi Kuu ya Tanzania Bara, ligi daraja la kwanza na la pili ambao watatakiwa kuwasiliana na meneja usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kupata maelezo ya kina ya namna ya kujiunga na mtandao wa GPX.

No comments: