Advertisements

Saturday, September 3, 2016

LIONEL MESSI KUUKOSA MCHEZO WA ARGENTINA DHIDI YA VENEZUELA

Mchezaji Lionel Messi atakosa mchezo wa kuwania kufuzu kutinga fainali za kombe la dunia baina ya Argentina na Venezuela, baada ya kuumia katika mchezo wa Alhamisi dhidi ya Uruguay.

Mshambuliaji huyo wa timu ya Barcelona, aliumia nyonga katika mchezo huo aliofunga goli moja lililoipa ushindi Argentina, baada ya kuamua kubadili uamuzi wake wa kustaafu kuichezea timu ya taifa.

Kocha wa Argentina Edgardo Bauza amesema Messi hatoweza kucheza mchezo na Venezuela jumanne ya wiki ijayo.

No comments: