Advertisements

Thursday, September 1, 2016

MAGUFULI ATISHIA KUBADILI NOTI KUWABANA WANAOFICHA FEDHA

Katika kile kinachoonekana kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha, Rais John Magufuli amesema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.
Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo mchana mjini hapa, Magufuli amesisitiza kuwa kauli hiyo ni mahsusi kwa watu walioficha fedha katika majumba yao na kuwataka kuachana na tabia hiyo mara moja ili fedha hizo ziingie katika mzunguko.
Huku akisisitiza kuwa katika utawala wake fedha za bure hazitakuwepo kwa sababu zilizokuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini ambazo kwa sasa zimedhibitiwa, alisema kwa mwendo anaokwenda nao sasa ni ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi.

CHANZO: MWANANCHI

4 comments:

Anonymous said...

Sawa mkuu wa nchi tumekusikia. Je hizo kazi ziko wapiwakati ikifika saa kumi jioni watu wanaanza kurejea makwao na hakuna wanaoenda makazini hadi kesho yake ukiacha walinzi, polisi, wanajeshi, airport isiyo na ndege na baadhi ya mahoteli ambayo sasaa hivi hayana wateja. Hebu acha kukurupuka weka ajira wazi na hela iwe kwenye mzunguko. Mamlaka itapeleka pagumu nchi mkuu!

Anonymous said...

Ni lazima puvu liwatoke.Magu is in a right track. Huwezi kubadili mfumo overnight acha aondoe mzunguko wa hela chafu ndio twende sawia.

Anonymous said...

Ushauri wa nia njema kabisa kwa Mhe. Rais. Umefanya kazi nzuri sana. Wengi wanayoitakia nchi yetu mema wanakuunga mkono. Unastahili kuungwa mkono kabisa. Lakini kuhusu kutishia kubadili fedha hapa unahitaji tahadhari kubwa sana. Fedha ni karatasi tu. Inategemea imani na kuaminiwa (trust and confidence). Iwapo watu watakosa imani nayo kwa vile kiongozi wa kisiasa anaweza kuibadili siku yeyote ile basi inaweza kuporomoka imani na hivyo thamani yake. Huko tusipajaribu. Tusije ishia kuwa na noti ya trlioni moja kama Zimbabwe na ambo hadi walilazimika kurudia dola ya mkoloni. vinginevyo mkuu ni kweli kabisa: watu wafanye kazi. peasa ya bure hakuna. Vijiwe haviwezi kutuendeleza. Sharti tutoe jasho. Hapa Kazi tu.

Anonymous said...

anon na 3 big up. umenena