Advertisements

Thursday, September 22, 2016

MKURUGENZI WA AFRIKA AKUTANA NA MABALOZI WA AFRIKA NCHINI KUZUNGUMZIA USHIRIKIANO

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samuel Shelukindo (kushoto) akizungumza katika kikao na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi za Afrika hapa nchini. Mazungumzo yao yalijikita katika kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na nchi zao. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Slipway iliyopo Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Septemba, 2016 
Sehemu ya Mabalozi kutoka nchi za Afrika wakiwa kwenye Mkutano wao na Balozi Shelukindo. Kutoka kulia ni Balozi wa Uganda hapa nchini, Mhe. Doroth Samali Hyuha, akifuatiwa na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Yasser El shawaf na Balozi wa Msumbiji, Mhe. Monica Patricio Mussa 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Bw. Suleiman Saleh wakati wa mkutano kati ya Wizara na Mabalozi wa Afrika waliopo nchini 
Mkutano ukiendelea.

No comments: