Advertisements

Thursday, September 15, 2016

MKUU WA MKOA WA KIGOMA AFUNGUZA RASMI WARSHA INAYOHUSU UBORESHAJI NA UANISHAJI WA MAHITAJI YA HUDUMA ZA HALI YA HEWA
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Brigedia jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga akifungua rasmi warsha hiyo kwa kusisitiza umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma hususani Ziwa Tanganyika wakati wa ufunguzi rasmi.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt. Hamza Kabelwa akielezea lengo la kufanyika kwa warsha hiyo ili kupunguza majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa kwa watumiaji wa Ziwa Tanganyika wakati wa ufunguzi rasmi.
Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Kanali M. M. Msuya akimkaribisha mgeni rasmi ili kuzungumza na wanawarsha wakati wa ufunguzi rasmi.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Brigedia jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha.

Warsha hii ya siku mbili imejumuisha wadau mbalimbali kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa; Uvuvi, Maafa na Usafirishaji, Wizara ya Maji; Bonde la Ziwa Tanganyika, SUMATRA, Bandari, Jeshi la Maji, Jeshi la Polisi, Kambi za wavuvi, Kambi za wasafirishaji (Beach Management Units), wanahabari na manahodha.

No comments: