Advertisements

Monday, September 19, 2016

NI MIAKA KUMI NA MITATU{13}ANAADHIMISHA KWA KULIPWA KIASI CHA SHILINGI 300 HUKU AKIPITIA CHANGAMOTO NGUMU ZA MAISHA KATIKA KUFIKIA NDOTO YAKE HIVI SASA.


Muandishi wa Habari muandamizi /ITV/RADIO ONE Mhe,Deogratias Macha

Na,Uvenal Kimario Writter

of Tupashane Habari Media Tanzania

Deogratias Macha?Ni Muandishi wa Habari Tanzania Pekee anayehudumia zaidi ya vituo kumi na moja vya Radio kwa wakati mmoja

Mfahamu...Alipo anzia...............Aliwahi kufanya kazi ya kuchimba mitaro kama Kibarua na kulimpwa shs 300/= ndizo zilizo mfanya afikie ndoto yake ,baada ya kudunduliza na pesa hizo zikamuwezesha kusoma chuo cha uandishi wa habari na utangazaji.

Ni mtu ambaye anaheshimu kazi kupita vyote,kutokana na mateso shida alizokutana nazo wakati akijitaidi kutafuta maisha yake mbali na wazazi.
Uliyafahamu haya kumhusu Mhe, Deogratias Macha? Ni Mwandishi wa habari mashuhuri wa Itv/Radio one Mkoani Kilimanjaro . Je, alifikaje? Na kabla alitokea wapi? Baada ya kumaliza mafunzo yake ya umeme wa viwandani katika chuo cha veta Moshi mkoani Kilimanjaro, alikutana na changamoto kadhaa hasa ya kukosa ajira kwa kipindi cha zaidi ya kipindi cha miaka mitano mfululizo.
”Nilimaliza mafunzo yangu mwaka 2002 kama mtaalamu wa umeme wa viwandani, kwa sasa labda ningekuwa nafanya kazi hiyo,” anasema Macha. Baada ya kumaliza chuo, juhudi za kusaka ajira zilikuwa ngumu.Kwa takribani mwaka mzima, ambapo baadaye alifanikiwa kupata kibarua katika kampuni ya Qeusem Ltd Arumeru Arusha inayo jihusisha na kilimo cha mbogamboga na matunda ambapo, badala ya kupangiwa kazi yake ya maswala ya umeme,alifanya kazi ya kuchimba mitaro kwa ajili ya ujenzi wa mashamba nyumba {Green house Effect} kwa ajili ya kupanda mbegu na kupitisha nyaya za umeme chini ya aridhi ,kwa kweli kazi hiyo haikuwa raisi kwake wakati huo kampuni hiyo inaanza ambapo alikuwa miongoni mwa vibarua waliokuwa wakifeka misitu na kuchimba mitaro, alibaki akishangaa ameomba kazi ya kufunga umeme anapewa kazi ya kuchimba mitaro na kufeka misitu,haikuwa rahisi aliwadanganya wazazi wake kuwa amefanikiwa kupata kazi aliyoisomea, ili wasiogope na wasimshauri aache kazi arudi nyumbani. “Hakukuwa na ajira na kishawishi cha kujiingiza katika uhalifu kilikuwa kikubwa endapo ningebaki mtaani na subiria ajira ya taaluma niliyo somea,” anasema bila kueleza zaidi.
Baada ya kushauriwa na mama yake kuendelea kusoma, alibana matumizi ya pesa huku akiwa anadunduliza kwa wakati huo alikuwa akilipwa shs 300/= kwa siku ambacho kilikua ni kiasi kidogo cha pesa, “Nilikuwa na Tembea kwa miguu kutoka eneo la kilala niliko kuwa , nimefadhiliwa na mama yangu mdogo Sr Mary Salome sehemu ya kuishi, kutokana na hali mbaya ya maisha yangu hali ambayo ilifanya niishi kwenye Kituo cha Afya Tumaini Kinacho milikiwa na masista wa kanisa katoliki“ sasa mimi ni kutoka kilala hadi chama QEUSEM LTD kwa miguu ni maisha ya ajabu sana kwa kuwa natembea kilomita25 na amka saa 10 usiku najitaidi kukimbia na kunasiku nili vamiwa na mbwa walinirarua kwenye tumbo na mshukuru mungu alininusuru na kifo pengine ningekufa,tukio linguine sita lisahau kunasiku kifua kilinibana nikiwa barabarani na elekea kazini nilijikuta nimeanguka katikati ya barabara tengeru,walio ni nusuru ni kinamama walikuwa wakiwahi sokoni ambapo walinibeba na kunipeleka hospital iliopo eneo hilo la tengeru, nimeamini Mungu yupo nami hadi leo pengine ningekuwa nimesha fariki .

Katika kipindi hicho Deogratias Macha Alimaarufu Babu Wa Vunjo anasema alikuwa akila chakula mara moja kwa siku kutokana na ugumu wa maisha . Mara baada ya kuona matumaini yakififia kupitia taaluma yake umeme wa viwandani aliamua kukusanya kiasi cha shs laki mbili na nusu iliyo tokana na shs 300 ambayo alikuwa analipwa kama malipo yake kwa siku na kumuomba mama yake Anna Temu Macha pamoja na Baba yake mzee Damiani Macha wa muongezee ili aendelee kusoma,
Macha aliamua kubadilisha ukurasa wa maisha baada ya kuacha kazi na kujiunga na chuo cha uandishi wa habari East African Training Institute, ambacho kwasasa inafahamika kama, The Arusha East African Training Institute “Mama yangu alikuwa wa kwanza kunijengea uwezo wa kuingia katika chuo cha uandishi wa habari , anapenda sana kusikiliza habari za redioni na alinishawishi kufuatilia kila habari iliyokuwa inaendelea duniani, nikawa na uwezo wa kutamka maneno vizuri na kusoma habari,” kufungua ukurasa mpya wa kuingia katika taaluma ya uandishi wa habari ukweli ni kwamba nilikuwa napenda sana taaluma hii tangu nikiwa Darasa la pili na nilivutiwa sana na Tiddo mhando kipindi hicho nikiwa na msikiliza Radio Tanzania , Joice Mwavile ,Marehemu Julias Nyaisanga, Abdul Ngarawa alikuwa mkurugenzi wa RTD,Deogratias Rweyunga , Charles Hilary ,Flora Nducha,Isaack Gamba pamoja na Taji liundi hawa ndio walio fanya niwe na juhudi ya kusoma”.

Mwaka 2004 alihitimu chuo cha uandishi wa Habari kwa ngazi ya cheti cha juu cha uandishi wa habari na utangazaji, alisoma kwa mwaka mmoja, Ilikuwa ni mwishoni mwenzi 30/1/2004, Macha alifanikiwa kupata kazi, kwa mara ya kwanza katika maisha yake ,katika kituo cha Radio 5Arusha Kama Mtangazaji na muandishi wa habari, kipindi hicho masikani ya kituo hicho yalikuwa kaloleni Arusha Katika Jengo La ccm Mkoa ‘’niliomba kufanya kazi bila malipo, nilipangiwa kusoma Habari, kuongoza kipindi cha Radio 5 na Matukio,Sauti ya Vijana na kumbuka pamoja na kipindi cha Wasanii chipukizi kilikuwa kikiitwa Arusha Babu Kubwa wakati mwingine nilikuwa naenda kutafuta habari,” anasema macha.,”
Deogratias Macha akiwa na mshauri wake wa vipindi vya siasa Radio 5, Mzee Malya ambaye sasa ni Marehemu.

Jambo la kujifunza hapa ni kwamba wakati mwingine katika kusaka ajira, kubali kufanya kazi bila ya malipo, onyesha jitihada zako, huenda ikawa ni njia nzuri ya kuajiriwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo yale ambayo huenda mtu amekwenda kwa ajili ya masomo kwa vitendo.

Aliamua kuendelea na masoma ya uandishi wa habari na utangazaji baada ya kuajiriwa mwaka 2006 katka kituo hicho, alijiunga na chuo cha uandishi wa habari Arusha Journalism Training College (A.J.TC) na kuendelea na mafunzo ya utangazaji,uandishi wa habari, uandaaji wa vipindi vya Radio na Tv kwa Ngazi ya Diploma wakati huo akiendelea kufanya Kazi Radio 5 Arusha,hadi alipo hitimu chuo 2008. “Hata hivyo mwaka 2009 walizuia mshahara wangu bila sababu yoyote kipindi hicho Radio ilikuwa imeuzwa kwa kampuni ya Tan media niliumia sana kwakuwa nilikuwa na majukumu yananitazama ,” anasema.
Wapili kushoto ni Mhe,Deogratias macha akiwa na waandishi wenzake katika kusherekea uhuru wa vyombo vya habari Duniani.

Wakati mwingine hata baya lina uzuri wake, macha hakuishia kulia mtaani, badala yake alianzisha mkakati wa kusaka ajira ambapo aliajiriwa kwenye kituo cha Upland Radio chenye makazi yake Njombe, kipindi hicho njombe ilikuwa na hadhi ya wilaya na sasa ni mkoa wa njombe alipofika kwenye kituo hicho alipewa nafasi , Msomaji wa Taarifa ya habari ,muandaaji wa vipindi vya kuhamasisha mapambano dhidi ya ukimwi, muongozaji na muandaaji wa vipindi vya jamii,” anasema Macha.

Nilidumu kwa mwaka mmoja kwenye kituo hicho cha Radio, Kila mahali kuna changamoto zake. “Mimi nikaondoka pale na kurudi tena Radio Five Arusha ,” anasema. Alipo Rudi Radio 5 Macha alifanikiwa kupata nafasi ya kazi chumba cha habari mpaka mwezi Agosti 2011 Baadae alihamia Sunrise Radio na Kupewa nafasi ya Manager wa Vipindi.
Deogratias Macha akiwa sunrise Radio-Arusha,Akisoma Taarifa ya Habari 2011.

Wakati huo Radio hiyo ilikuwa Katika majaribio baada ya kununuliwa Aspire Media Co.Ltd alikuwa miongoni mwa wataalamu katika timu maalumu ya kuunda vipindi, alifanya vipindi vya Hii leo,Siku mpya na kusoma habari.

”Nilipenda niendeleo kuangaika ili nitimize ndoto yangu ya kuwa muandishi wa habari na mtangazaji mwenye uwezo kama walionipa moyo hadi nikaipenda zaidi taaluma hii.”

niliandika barua mara ishirini ITV/Radio One sikuwahi kufanikiwa kupata nafasi ya kazi, Mwaka 2014 nilijaribu tena kuandika barua ya kuomba nafasi ya uandishi wa habari ITV/RADIO ONE KATIKA Mkoa wa Kilimanjaro hatimaye Mungu mkuu hachelewi wala hawai alinitendea matendo yake makuu nami nikamwona kwa jinsi ya ajabu kweli nilifanikiwa na kuitwa kwajili ya kufanyiwa usahili na hatimaye nikawa mmoja wa wanafamlia wa ITV /RADIO ONE”hali ambayo iliyonifanya ni achane na Sunrise Radio .

Akiwa muwakilishi wa Radio one/ITV Deogratias macha anatuma taarifa zake katika kipindi cha Nipashe Kinacho Sikika Kuanzia majira ya saa6:30Asubuhi hadi saa6:55 Asubuhi,kipindi cha mambo mseto Kinacho Rushwa na Radio One Jumapili saa 21:00usiku hadi 21:55 usiku,kipindi cha miwani ya Maisha Kinacho sikika jumamosi saa 10:00Asubuh-saa 12:00mchana ,Kipindi cha Duru Zetu Kuanzia saa 21:00 Usiku siku ya jumanne na jumatano,ni baadhi ya vipindi anavyo tuma ripoti zake kutoka Mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wa ITV ,Deogratias Macha amekuwa akituma taarifa zake kwa baadhi ya vipindi vya habari.
Baadhi ya picha hapo juu,zikimuonyesha Mhe,Deogratias macha akiwa na wezake katika majukumu ya taifa matukio haya akiwa Radio five na Sunrise Radio.

Deogratias Macha amewahi kushinda Tuzo nyingi ikiwemo tuzo ya Baraza la Habari Tanzania Mct ,baada ya kushindanisha kazi zake ,Mnamo tarehe 14/3/2013 hali iliyompelekea kushinda tuzo ya muandishi bora wa habari za Jinsia,
Mhe,Deogratias Macha akizungumza na Mratibu wa Jeshi la Polisi na mkuu wa kitengo cha polisi jamii na dawati la jinsia na wanawake Mkoa wa Arusha Afande Mary Lugola.

Kutokana na kujituma na kufanya kazi zenye ubora,ameendelea kupata umarufu zaidi, baadhi ya vituo vya Radio vimekuwa vikiingia naye mkataba wa kazi,licha ya Kufanya kazi ITV/RADIO ONE.,

Ukweli unao julikana Macha ni mwandishi pekee Tanzania anaye ongoza kufanya kazi na zaidi ya vituo kumi na moja vya radio.

Yeye anasema hayo ni majibu ya maombi yake ya nyuma,na mungu amejibu baada ya wakati kufika yani wakati ndio huu, kwakua ni muda mrefu amemuomba mungu,kapiga magoti kwelikweli na kuomba hadi sasa amejibiwa maombi yake,kutokana na hivyo basi anasema kama kazi inamlipa na hakiuki sheria za nchi ataifanya kwa moyo wote,na kuwa hawezi kukataa kazi wala kukata tamaa kwa kuwa Mungu ndiyo tegemeo lake daima.
UNAFANYA VIPI KAZI ZAIDI YA VITUO KUMI NA MMOJA KWA SIKU.

“Unaweza ukaona ni ngumu sana na unachukua muda mwingi sana,kwangu mimi cha msingi ni muda, ninaamka saa 11 alfajiri nikiwa naelewa ratiba zangu bila ya kuadhiri hata moja,nakwenda vijijini kukutana na wananchi na kuzungumza nao changamoto zilizopo, nafanya nao mahojiano na kuakikisha kwa siku nina tarifa mpya zaidi ya kumi . natuma kila moja inapo takiwa kwenda kwa njia ya barua pepe.

Picha hapo juu,Wapili kulia Mhe,Deogratias Macha wakwanza kulia ni Alfonce Tonn watatu Clara Moita anaye fuata Devi Rwenyagira wakati akiwa anafanyakazi Radio 5Arusha.

Deogratias macha amesema anamda mchache sana wakuwa karibu na marafiki kwa kiasi kikubwa anawatumia muda wake kufanya kazi.

Anasema siri ya kukubalika na kuaminika na kupewa nafasi nyingi za kazi ni kutokana na kujituma kwenye kazi, ambapo amewataka vijana kujituma na kuwa na malengo.
Vituo vya Radio alivyo ingia navyo mkataba wa Kazi hadi sasa licha ya kuwa ITV/RADIO ONE.Swaiba Fm –Zanzibar muandishi wa makala ya amka nasi.Redio sauti ya Injili-Moshi muandishi wa makala ya Dira,Fountain Radio fm-,Muandishi wa habari na mtangazaji.Kibo Fm.Msomaji wa habari.

Tupashane Habari Radio online-Moshi www.tupashanehabari.blogspot.com, Muandishi wa habari na mtangazaji.

Hivi ni baadhi ya vituo vya Radio ambavyo anavifanyia kazi,mhe,Deogratias ni mwalimu wa chuo cha uandishi wa habari Tupashane habari College Moshi.

MAFANIKIO KWA KIPINDI KIREFU HADI SASA.
Deogratias macha ni mmiliki wa taasisi ya Tupashane Habari Media Tanzania,Taasisi hii inashughulika na mambo mengi,ambapo inamiliki Tupashane Habari College –Tanzania chuo hiki kipo moshi mjini manyema mbuyuni Kwa maelezo tembelea www.tupashanehabaricollege.blogspot.com kwa taarifa kuhusu chuo .

Chuo hiki kinatoa mafuzo ya uandishi wa habari na utangazaji sambamba na kozi mabalimbali,anasema chuo hiki kinamwaandaa pia mwanafunzi kujiajiri.

Pia anamiliki Tanzania Media Tv,ambayo inarusha matangazo kwa njia ya mtandaoni {online tv}kupitia u-tube channel,Tupashane Habari Rado online inapatikana www.tupashanehabari.blogspot.com.

Mpango wako wa badaye ni hupi.

“Nategemea kuwa mtangazaji wa Radio one,unaweza ukashanga kwanini bado na tamani kwenda makao makuu,ninahitaji kufanya kitu cha tofouti,hapa nilipo sitaweza kufanya kwakuwa sina nafasi ya kubuni kitu kama ninavyo taka sijui umenielewa,” Kubwa analo lenga mhe,Deogratiasi Macha ni nafasi ya ubunifu wa vipindi ambavyo vitawezesha kuteka soko la biashara Radio one, anavyo amini yeye vipindi vyenye ubora husikilizwa na wengi na hata kuwafanya wateja kutangaza biashara zao na kituo cha Radio. “Radio one vipindi vyake vyote ni vizuri sana, nina kitu nataka niboreshe viendelee kuwa vizuri zaidi,naaminikuna siku nitakuwepo hapo kwakuwa mungu ameshafanya njia’’.
Anasema ndoto yake ni kuwa muandishi wa habari wa kimataifa.Pia anamipango ya kuwania ubunge kati ya majimbo

mawili ambayo anamahusiano nayo kwa ukaribu,majimbo hayo ni moshi vijijini na Jimbo la vunjo,mwaka 2015 alitaka kutangaza nia ya kugombea kati ya jimbo mojawapo,ambapo aliombwa na mmoja wa mgombea asubiri kwanza kwa makubaliano maalumu,kwa sasa aijulikani kama Deogratias Macha atajikita kwenye siasa baada ya kujishughulisha sana na maswala ya kijamii

ULIWAHI KUFANYA KAZI NA MWANASIASA?

Ndio....

HAPA DEOGRATIAS MACHA ALIWACHEKESHA WATU NI BAADA YA KUKUBALI KUWA MSHAURI WA ALIYE WAHI KUWA MBUGE WA VYUNJO KATIKA MASWALA YA HABARI NA MAWASILIANO.
Deogratias Macha wa Kwanza kushoto,anaye fuatia wapili ni Mhe,Agustino Lyatonga Mrema na wa nne kulia ni mke wa mhe mrema mama mrema,Picha ni kwa hisani ya www.tupashanehabari.blogspot.com

Deogratias alitumika kuandaa taarifa mbalimbali kama alivyo kuwa akifanya kwa vyama vingine vya siasa, kwa upande wa Tlp alimshauri Mhe mrema asigombee ubunge kwa sasa na badala yake akabidhi nafasi hiyo kwa baadhi ya wanachama wa Tlp.

”Mhe kwakweli wananchi wake wanampenda sana tatizo ni kwamba ni mtu ambaye akikatishwa tamaa anatumia vizuri nafasi hiyo, kwa lengo la kutengeneza hoja ili aweze kuendelea na mpango wake, tatizo alama za nyakati hakusoma mapema, tulikosana baada ya kumshauri asigombee alidhani nilitumiwa ili nimmalize kisiasa,sikushangaa kwakuwa nihaki yake kufikiri nimetumiwa,mimi nilipenda apumzike kwakuwa kafanya mengi mazuri ndani ya jimbo la vunjo na Tanzania kwa ujumla ni miongoni mwawasiasa mkogwe nchini ninaye mkubali alisema Macha”.

Deogratias macha kunawakati alikuwa akimzungumzia mhe mrema kama mtu mwenye moyo wa makusudi wa kujiumiza baada ya kutangaza kugombea ubunge jimbo la vunjo mwaka 2015,

Mrema ni mwanasiasa mkongwe ambaye nimebahatika kufanya nae kazi kwa kipindi kirefu nikiwa nafanya kazi nje ya Mkoa wa Kilimanjaro,nimejifunza mengi mazuri kutoka kwake.

Deogratias Macha anasema mhe wakati akiwa mbunge wa Jimbo la vunjo aliwahudumia wananchi wake vizuri , kushindwa kwake ubunge sio kwamba akubaliki kwa wananchi Laa! waliamua apumzike na bado wanampenda usishangae baadae atangaze kurudi tena na kushinda ubunge, hakufanya baya bali mazuri yanaonekana.

Ukiteuliwa na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli kuwa mbunge, Utawafanyia nini wananchi tofouti na Wabunge walioko bungeni hivi sasa?

Kwanza sijawahi kufikiria kuteuliwa na Rais kwenye nyadhifa yoyote nchini na wala sitakaa kufikiria, kwakua ni sawa na kungoja miujiza badala ya kujituma ufikie lengo kwa wenzetu wazungu wanasema don’t wait The Perfect Moment but take it the moment and make it Perfect,na mimi siyo mtu wakungoja miujiza kwa kuwa inaweza isitimie kwangu .

Maisha yako kwa ufupi

Mimi mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu,wa familya ya Mzee Damiani G. Macha na Bibi Anna Temu Macha mama yangu ni muuguzi wa hospital ya Kcmc na baba ni mstaafu, awali alikuwa muajiriwa wa kiwanda cha kahawa mjini moshi {KNCU} na sasa anajishughulisha na kilimo na ufugaji,Nina wadogo zangu wawili Hilda na Silvia.

Deogratias Macha amefunga Ndoa na Glory mwaka 2007 na wanawatoto watatu, Mary,Deodatus na Dayana,Mke wake awali alikuwa ni Mwalimu wa secondary sasa ni Afisa mstawi wa jamii.Deogratias Macha Amezaliwa mwaka 1982 Moshi, Amesoma shule ya msingi Moshi na baada ya kuhitimu aliendelea na elimu yake ya secondary katika shule ya Lombeta sec. iliyopo Kilema na kwasasa ni mwanachuo wa chuo kikuu Uria

Unatumia Mtandao wa simu wa aina gani?

Mimi situmii mtandao,bali mitandao ni kimaanisha ni mingi kutokana na shughuli zangu ninazo fanya....

Mtandao wa vodacom, nawasiliana na mtu yoyote Yule 0756483 174 kwa ajili ya kazi nyingine.

Historia hii nimeweza kufanya mahojiano na Mhe:Deogratias Macha ambaye ni nguli wa tasnia ya Uandishi wa habari na utangazaji Nchini Tanzania kutokana na kumbukumbu yake anayoiadhimisha kila ifikapo tarehe 16/09 kila mwaka ambapo anakumbuka mwaka 2003 aliachana na kazi ngumu ya uchimbaji wa mitaro na kujiunga na chuo cha uandishi wa habari kutokana na juhudi zake binafsi za kuokoteza/kudunduliza kama waswahili wasemavyo haba na haba hujaza kibaba ndivyo ilivyokuwa kwake alilipwa shilingi 300 fedha ya kitanzania kwa siku ndiposa kufikia malengo na ndoto zake.

Hiyo ndiyo historia fupi katika kumfahamu Mhe:Deogratias Macha.

No comments: