Advertisements

Saturday, September 3, 2016

PICHA: WASANII WA WCB WALIVYOPOKELEWA KWA SHANGWE LODWAR, KENYA

 Siku mbili zilizopita wasanii wa lebo ya WCB, Harmonize, Raymond na Rich Mavoko waliwasili nchini Kenya kwa ajili ya kufanya show nchini humo pamoja na kufanya ziara kwenye vituo mbalimbali vya habari vilivyopo huko.

Wasanii hao walipata mapokezi ya heshima mjini Lodwar, Kenya japo siyo rahisi kwa wasanii kama wao ambao hawana muda mrefu kwenye muziki kutegemea kufanyiwa hivyo japo Rich Mavoka inadaiwa kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa Bongo wanaokubalika nchini humo.

Wananchi wa mji huo wanaonekana kuwakubali zaidi wasanii wa Bongo ikiwa ni wiki mbili zilizopita Mr Nice alifanikiwa kupata mapokezi ya kishindo kwenye mji huo huo. Wasanii hao walifankiwa kufanya show usiku wa jana, Septemba 2 kwenye ukumbi wa Home Land Club.

No comments: