ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 5, 2016

WIZARA YA AFYA YASISITIZA JUU YA MATUMIZI SAHIHI NA ENDELEVU YA KONDOM MPYA YA ZANA

Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro (katikati), akizungumza kwenye semina elekezi kuhusu uzinduzi wa Kondom mpya ya Zana itakayokuwa ikitolewa bure na serikali kwa wananchi, iliyofanyika Jijini Mwanza leo.Na BMG

Washirki wa semina hiyo
Wanasemina
Wanasemina
Mmoja wa washiriki wa semina akihojiwa na wanahabari
Mmoja wa washiriki wa semina akihojiwa na wanahabari
Picha ya pamoja

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewahimiza wananchi kuzingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondomu ili kujiepusha na mimba zisizotarajiwa pamoja na magongwa ya kuambukiza ikiwemo virusi vya Ukimwi.

Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro, ametoa rai hiyo hii leo Jijini Mwanza, kwenye semina elekezi kuhusu uzinduzi wa Kondom mpya ya Zana itakayokuwa ikitolewa bure na serikali kwa wananchi.

Katikiro amesisitiza matumizi sahihi na endelevu ya kondom ya Zana kwa wananchi walio kwenye mahusiano ya kimapenzi, yatasaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama virusi vya Ukimwi pamoja na mimba zisizotarajiwa na kwamba aina hiyo ya kondom ni imara na yenye ubora.

Mratibu wa mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, mkoani Mwanza, Geofrey Mabu, amesema mkoa wa Mwanza umejipanga vyema ili kuhakikisha kondom za Zana zinawafikiwa walengwa hususani kupatikana bure katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye vituo vyote vya afya, maeneo ya starehe pamoja na kwenye ofisi za serikali na binafsi.

Uzinduzi wa Zana Kondom kitaifa ulifanyika mkoani Mbeya wiki iliyopita ambapo kwa mkoa wa Mwanza uzinduzi utafanyika kesho Jijini Mwanza ambapo aina hiyo ya kondomu itakuwa mbadala wa kondom za MSD zilizokuwa zikitolewa pia bure na Serikali lengo likiwa ni kuhakikisha mapambano dhidi ya Ukimwi yanafanikiwa.

Bonyeza HAPA Kujua Zaidi

No comments: