Advertisements

Monday, October 17, 2016

HARUSI YA BEKA NA NASRA

Bakari Makuka ‘Beka’ na mkewe Nasra wakiserebuka wakati wa harusi yao.
Beka akionyesha umahiri wake katika kusakata rhumba.
Burudani zikiendelea wakati wa harusi hiyo ambayo wasanii wengi waliisusia.
Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye alikuwa bestman (kushoto) katika pozi na bibi harusi.
Bibi harusi, Nasra naye akisakata rhumba wakati wa sherehe hizo.
Nasra katika pozi.
Wageni waalikwa wakitoa mkono wa shukrani kwa maharusi.
Maharusi katika pozi.
Maharusi pamoja na wanakamati wakipozi wakati wa harusi hiyo.
MC wa sherehe hiyo, Dk. Cheni akiwa kazini.
Maharusi wakitoka ukumbini baada ya shughuli.

Jana ilikuwa ni siku ya sherehe ya ndoa ya msanii wa filamu Bongo, Bakari Makuka ‘Beka’ ambapo ilifana vilivyo huku waalikwa wakila, kunywa na kuserebuka vilivyo.

Sherehe hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Prime Rose uliopo Mbezi Beach, Dar ikiwa ni baada ya kufunga ndoa na mkewe Nasra, Ijumaa iliyopita katika msikiti wa Ununio, Jumamosi ikafuatiwa na sherehe ya Maulid nyumbani kwao Beka, Sinza, Dar.

Katika sherehe hiyo mastaa wenzake ni kama walisusia kwani aliyekuwepo ni Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye alikuwa bestman na Dk. Cheni ambaye alikuwa mshehereshaji jambo ambalo liliwashangaza baadhi ya wageni waalikwa kwani siyo kawaida ya wasanii kutotokea kwenye shughuli kama hiyo.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo kwa nini wasanii wenzake hawakujitokeza, Beka alisema;

“Kiukweli hata mimi nashangaa maana nimewaalika wasanii wote lakini hawajaja sijui kwa nini.”

No comments: