Advertisements

Monday, October 3, 2016

MAALIM SEIF AIHOFIA OFISI YA BUGURUNI

By Beatrice Moses bmoses@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi wa muda CUF Julius Mtatiro amesema Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharrif Hamadi hawezi kufika Buguruni kwa kuwa si salama.

Mtatiro alisema wataendelea kukutana na kufanya mikutano yao katika maeneo ya nje ya Ofisi ya Buguruni hadi hapo hali itakapokuwa shwari.

Mtatiro alisisitiza kuwa chama hicho kipo imara na wataendelea kudumisha amani na mshikamano.

Mkutano huo wa viongozi wa CUF ulifanyika katika hoteli ya Peacock leo, jijini hapa.

No comments: