Advertisements

Monday, October 24, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) ,Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam .

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) aliyemtembelea na kufanya naye mazungumzo  ,Ikulu jijini Dar es Salaam


                               .....................................................................
Balozi wa Italia hapa nchini Tanzania Roberto Mengoni amemhakikishia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa nchi yake itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri na ya kihistoria kati ya nchi hizi mbili katika sekta mbalimbali kama hatua ya kuongeza chachu ya maendeleo kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.

Balozi huyo wa Italia hapa nchini ametoa kauli hiyo leo 24-Okt-2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi huyo Roberto Mengoni ameeleza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana ipasavyo na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya,utamaduni na elimu.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kusaidia miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya hapa nchini.

Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Italia katika sekta mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa biashara na shughuli za utalii kati ya Italia na Tanzania.
Amesisitiza kuwa Serikali ipo tayari wakati wowote kupokea mawazo mazuri ya kimaendeleo kutoka kwa Serikali ya Italia yatakayosaidia kujenga na kuimarisha ustawi mzuri katika jamii hapa nchini.

No comments: