Advertisements

Friday, October 21, 2016

Malkia meno ya tembo, wenzake wadaiwa kukiri makosa

By Tausi Ally, Mwananchi tally@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Washtakiwa watatu, akiwamo raia wa China, Yang Feng Glan (66) maarufu kama malkia wa meno ya tembo wamedaiwa kukiri makosa wakati wakihojiwa polisi.

Feng na wenzake wanadaiwa kusafirisha meno hayo yenye thamani ya Sh5.4 bilioni.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa hayo jana na Mawakili wa Serikali, Paul Kadushi na Faraja Nchimbi.

Imeelezwa kuwa katika usikilizwaji wa kesi hiyo utakaofanyika Novemba 4 na 15 wanatarajia kuita mashahidi wasiopungua tisa.

Washtakiwa wengine ni Salvius Matembo (35)na Manase Philemon (39) ambao wanatetewa na mawakili Masumbuko Lamwai na Nehemia Nkoko.

No comments: