Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akijionea kiatu aina ya Safari buti kinachozalishwa na Kiwanda cha Karanga kilichopo Mkoani Kilimanjaro wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kiwandani katika Mkoa huo. Masauni amesisitiza kiwanda hicho kuzalisha bidhaa bora zaidi ili kuteka soko kubwa zaidi pamoja na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo. Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho Mrakibu Msaidizi, Michel Minja na kushoto ni Ali Jambaraga Fundi Mkuu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akiangalia kiatu kilichokuwa tayari kuvaliwa kilichotengenezwa katika kiwanda cha Karanga kilichopo Gereza Kuu la Karaga mkoani Kilimanjaro. Naibu Waziri huyo amesisitiza Jeshi hilo kuzidi kutengeneza bidhaa bora zaidi za viatu ili kuhakikisha wanapata soko kubwa ndani nan je ya nchi., kulia ni Kamishan Msaidizi Mwandamizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa aliye aambatana nae kwenye ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun (aliyevaa koti) akitoa maelekezo kwa Wakuu wa Gereza la Karanga na kiwanda cha Viatu kilichopo gerezani hapo. Masauni amelitaka jeshi hilo kuzidi kutoa bidhaa bora ili kuendelea kuteka soko kubwa ndani nan je ya nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Hamad Masauni, (mwenye tisheti nyekundu) akielekea kutizama mpaka wa Tarekea wilayani Rombo ili kujionea changamoto zinazotokana na mipaka hiyo pamoja na kutoa maagizo kwa viongozi wanaohusika kuimarisha ulinzi wa mpaka huo ili kukabiliana na upitishaji wa bidhaa za magendo pamoja na wahamiaji haramu ambao wamekua wakiinia nchini bila vibali. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimaanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wilbrod Muutafungwa akifatiwa na Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanguku, na wan ne kutokea kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo Agnes Hokororo alieambatana na Naibu Waziri huyo kuangalia mipaka hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimajaro alipotembela mpaka wa Tarakea wilayani Rombo Naibu waziri Masauni amesema kuwa licha ya changamoto zinazojitokeza katika mipaka yote miwili ni lazima kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye mipaka hiyo na kudhibiti njia zote zisizo rasmi zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja na wafanyabiashara za magendo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun akipewa maelezo na Afisa Mipaka Holili Michel Amo, juu ya jiwe linaloonyesha mpaka wa Tanzania na Kenya lililopo katika mpaka wa Holili ambalo limekua likisogezwa na watu wasiojulikana hivyo kuharibu alama za mipaka. Naibu waziri Masauni amesema kuwa licha ya changamoto zinazojitokeza katika mipaka yote miwili ni lazima kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye mipaka hiyo na kudhibiti njia zote zisizo rasmi zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja na wafanyabiashara za magendo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipowasili katika Gereza Kuu la Karanga, Mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea kiwanda cha viatu kilichopo gerezani haapo ili kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali hasa viatu. Naibu Waziri huyo amelitaka Jeshi hilo kuzidi kuboresha bidhaa za viatu hivyo ili kujipatia soko kubwa ndanni ya nchi na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanattumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akisalimiana na Mkuu wa Gereza la Karanga, Kamishna Msaaidizi Mkwiche mkoani Kilimanjaro wakati alipofanya ziara katikaa Kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo ili kujionea uzalishaji wa bidhaa za viatu ambavyo Rais Magufuli alitaka majeshi yote nchini kutumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akisikiliza maelezo kuhusu uzalishaji wa viatu katika kIwanda cha Gereza la Karanga kutoka kwa Fundi Mkuu wa Kiwanda hicho Ali Jambaraga wakati alipofanya ziara yake kwenda kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali lakini pia ametaka wazidi kuzalisha bidhaa bora zaidi ili kuteka soko la ndani na je ya nchi ikiwa ni pamoja na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini kutumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun aagiza Jeshi la Magereza kuzidi kuboresha viatu vinavyotengenezwa na kiwanda chao ili kujipatia soko kubwa ndani ya nchi na nje.
Hayo aliyasema jana kwa wakuu wa Gereza la karanga na viongozi wa kiwanda hicho alipofanya ziara yake ya siku moja katika kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo, mkoani Kilimanjaro
Aidha, Naibu Waziri huyo alisisistiza Jeshi hilo kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi la Magereza, hivyo ni muhimu kuendelea kuzalisha bidhaa zilizo bora zaidi
Haiingii akilini maofisa wa majeshi mbalimbali nchini kuagiza viatu nje ya nchi wakati viwanda vya ndani vinauwezo wa kuzalisha viatu bora zaidi vinavyodumu kwa muda mrefu kuliko vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi, alisema Masauni.
Masauni alisema kwamba dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kati hivyo Jeshi la Magerezaa kupitia kiwanda chake na miradi mingine mingi halina budi kuendelea kuzidisha kuzalisha viatu bora vitakavyo kidhi kiwango cha uhitaji na soko ili kukuza uchumi wao na Serikali kwa ujumla.
Aidha, katika ziara yake, Naibu Waziri Masauni amesisitiza kuwa ni muhimu Jeshi hilo kufanya miradi mingi kwa ustadi mkubwa ili kujipatia psa zitakazosaidia kujiendesha wao kama jeshi na mashirika mengine yanayounga mkono miradi yao hivyo kutotegemea ruzuku kutoka serikalini.
Waziri huyo alilipongeza Jeshi hilo kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora kulinganisha na nyingine zinazoingizwa nchi, hivyo amesisitiza kuzidi kutengeneza viatu bora zaidi ili kuwa na uwanja mpana wa soko la ndani nan je ya nchi.
No comments:
Post a Comment